Na Mbuke Shilagi Kagera. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imesema ushirikishwaji wa wadau katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni silaha muhimu ya kuzuia rushwa, ucheleweshaji wa miradi na matumizi mabaya ya fedha za umma.
Akizungumza wakati wa warsha ya wajibu wa wadau katika usimamizi na utekelezaji wa programu na miradi ya maendeleo, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera Ismail Bukuku amesema miradi inayotekelezwa bila kuwashirikisha wadau hukosa uwazi na huwapa nafasi wahusika kufanya ubadhirifu.
Bukuku ameeleza kuwa mfumo wa Public Expenditure Tracking System (PETS) unalenga kuhakikisha fedha za umma zinatoa thamani halisi kwa kuzingatia ubora wa miradi, manufaa kwa wananchi na matumizi sahihi ya rasilimali za Serikali.
Amesema PETS pia husaidia kuzuia uvujaji wa fedha, ucheleweshaji wa miradi, kushuka kwa ubora wa kazi pamoja na vitendo vya rushwa vinavyoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa TAKUKURU, kuanzia mwaka 2023 hadi 2026, taasisi hiyo imefuatilia jumla ya miradi 258 katika Mkoa wa Kagera ambapo miradi 26 ilibainika kuwa na viashiria vya rushwa. Pia taasisi hiyo ilitoa mapendekezo ya maboresho katika miradi 207 na kutekeleza programu 242 za uelimishaji na uhamasishaji kwa wananchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahaya Ramadhani Kido, amesema Serikali inatarajia kuona kila mdau anasimamia kwa karibu miradi inayotekelezwa katika eneo lake na kuchukua hatua za haraka pindi changamoto zinapojitokeza.

Social Plugin