Na Sheila Ahmadi, Bahi
Serikali inaendelea kuboresha Huduma za usafirishaji wa Reli ya Mizigo kutoka Dare salaam hadi Bahi ikiwa imefikia asilimia 98 ya utekelezaji.
Akizungumza Mkoani Dodoma na wanahabari kwenye stesheni ya Mizigo bahi Mhandisi wa mradi wa kipande cha pili cha stesheni ya SGR ya mizigo kutoka Dar es salaam hadi Makutupora Christina Samweli amesema kufikia sasa mradi wetu uko Mwishoni kukamilika huku Mkandarasi akiwa amefikia asilimia 98% hivyo tunaanza kuendesha treni ya mizigo kutoka Daresalaam hadi kufika Bahi mkoani Dodoma.
Tumeanza kusafirisha Mizigo kutoka kwenye Bandari ya Dar es salaam hadi Stesheni ya Bahi ambapo ina uwezo wa kupokea Makasha 1500 kwa Wakati Mmoja huku tukisafirisha kwa SGR na kuhamishia kwenye Reli ya Zamani MGR kwenda Mwanza,Isaka na Kigoma.
"Nitoe wito kwa wadau Wote nchini wanaosafirisha mizigo watumie usafiri wa reli kwani usafiri wa Reli ni Waharaka na salama Zaidi ambapo unatumia muda mchache wa masaa Matano kwenye kusafirisha mizigo. "Amesema Mhandisi Samweli.
Aidha katika kutumia Reli ya Mizigo kutapunguza uharibifu wa Miundombinu ya barabara hivyo barabara hizo zitakuwa salama ambapo zinasababishwa na uzito wa mizigo huku kupitia treni hiyo behewa moja linasafirisha Tani 56 ambapo lina makasha Mawili huku kila kasha likiwa limebeba Tani 28.
Katika Hatua nyingine tunawakaribisha wasafirishaji wote wanaotumia malori kwani kutapunguza muda mwingi wa kusafiri barabarani sisi tutachukua mizigo na kusafirisha kwenye reli kutoka Mikoa ya kigoma, Tabora na kuleta bahi na kwenda kusafirisha Daresalaam kwa kutumia SGR.




Social Plugin