Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MSHAHARA WA KWANZA WA ASKARI WAPYA RUKWA FUNGU LA KUMI LATUA KWA WENYE UHITAJI


Na Mwandishi wetu,Rukwa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limeendelea kuimarisha dhana ya Polisi Jamii kwa kuwagusa watoto wenye mahitaji maalum wanaosoma katika Shule ya Msingi Malangali iliyopo Manispaa ya Sumbawanga, kupitia msaada wa vifaa na vyakula vilivyotolewa na Askari wapya wa Depo Na. K 3 waliotenga sehemu ya mshahara wao wa kwanza baada ya kuajiruwa kwa ajili ya kusaidia watoto hao.

Msaada huo ulikabidhiwa Julai 15, 2026 katika hafla iliyoongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, SACP Shadrack Masija, na kuhudhuriwa na Wakuu wa Polisi wa Wilaya, Maafisa, Wakaguzi pamoja na askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Kamanda Masija alisema hatua hiyo ni sehemu ya kuimarisha uhusiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii, huku akiwataka askari kuendelea kuwa karibu na wananchi kwa kushiriki shughuli zenye manufaa kwa makundi yenye uhitaji.

Kwa upande wao, walimu wa Shule ya Msingi Malangali walilishukuru Jeshi la Polisi kwa msaada huo pamoja na elimu waliyotoa kwa wanafunzi, wakieleza kuwa kitendo hicho kimeongeza furaha, matumaini na kuwafanya watoto kujiona kuwa sehemu muhimu ya jamii. Nao wanafunzi walionesha shukrani zao kupitia nyimbo na salamu maalum walizowaimbia askari hao, wakieleza furaha yao kwa upendo walioupokea kutoka kwao.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com