Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU CCM AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA


Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Dkt. Asha-Rose Migiro, amefanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Julai 15,2026, viongozi hao walijadiliana kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Ufalme wa Norway, pamoja na maeneo ya ushirikiano yanayohusu maendeleo ya kidemokrasia, utawala bora, ujenzi wa taasisi na maendeleo endelevu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com