Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA KITAIFA YA UFUNGAJI MIGODI YAKAGUA MPANGO WA UFUNGAJI MGODI WA BARRICK BULYANHULU

Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa Barrick Bulyanhulu, Agapit Paul, akitoa maelezo kuhusu shughuli za uendeshaji wa mgodi kwa wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ufungaji Migodi (NMCC) wakati wa ziara yao ya kikazi mgodini.
Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa Barrick Bulyanhulu, Agapit Paul, akitoa maelezo kuhusu shughuli za uendeshaji wa mgodi kwa wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ufungaji Migodi (NMCC) wakati wa ziara yao ya kikazi mgodini
Viongozi na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ufungaji Migodi (NMCC) wakisikiliza maelezo kuhusu shughuli za uendeshaji wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu wakati wa ziara yao ya kikazi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Ufungaji wa Migodi nchini , Mhandisi Hamisi Kamando (mwenye fulana nyeusi ) akisisitiza jambo kwenye ziara ya siku mbili ya kamati hiyo kwenye mgodi wa Barrick Bulyanhulu , kulia kwake ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Rhys Harvey na wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga , CP Salum Rashid Hamduni na mwisho kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhandisi Ephraim Mushi.
Mwenyekiti wa kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi nchini akitoa majumuisho ya ziara ya Kamati kwenye mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Meneja Mkuu wa Barrick Bulyanhulu Rhys Harvey akiongea katika Mkutano wa ujumbe huo uliofanya ziara ya kikazi mgodini
Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa Barrick Bulyanhulu Agapit Paul akitoa ufafanuzi wa masuala ya uendeshaji wa Mgodi huo
Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick katika kikao kazi hicho
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga , CP Salum Rashid Hamduni akizungumza.

  ***

#Yapongeza Barrick kwa uzingatiaji wa sera, kanuni na sheria za nchi


Kamati ya kitaifa ya Ufungaji wa Migodi nchini imesema imeridhishwa na mchango wa kampuni Barrick nchini inayoendesha shughuli zake kwa ubi ana serikali kupitia kampuni ya Twiga kwa uendeshaji shughuli zake kwa weredi mkubwa ambao unafanikisha ukuzaji wa Uchumi wa taifa kupitia ulipaji wa kodi, ushuru, gawio la hisa na uchagiaji kwenye maendeleo ya wananchi wanaozunguka migodi hiyo kupitia miradi inayotekelezwa kwa fedha za CSR na sera ya maudhui ya ndani (Local content).

Akifunga na kutoa majumuisho ya ziara ya siku mbili ya wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ufungaji wa Migodi nchini, ambayo ilitembelea Mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo Wilayani Msalala Mkoani Shinyanga, Mwenyekiti wake, Mhandisi Hamisi Kamando, amesema imeridhishwa na taarifa za mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa uzingatiaji wa kanuni na weledi wa uendeshaji wa mgodi huo.

“Sisi tumepewa malengo na serikali ya kukusanya fedha kwenye sekta hii ila tunawashukuru sana kwa mchango wenu kwenye maendeleo na ustawi wa watanzania kwa ujumla tumeona kwenye sera na kanuni za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) mnafanya vizuri,”

“Mnachohitaji ni kuwezeshwa kwa kuwekewa mazingira mazuri (facilitation) ya kufanya kazi vizuri zaidi katika sekta hii ya madini nchini ili serikali iendelee kukusanya mapato kwa maslahi ya taifa kwa ujumla,” amesema Mhandishi Kamando.

Ameongeza kwamba katika mipango ya baadaye ya ufungaji wa mgodi huo wa Barrick Bulyanhulu ambao umehuishwa maisha hadi 2050 ni mipango ambayo imekaa vizuri ambapo inahitaji marekebisho madogo ili kuendana na sheria , kanuni na maelekezo ya serikali.

Mhandishi amefafanua kuwa ni muhimu kwa Mgodi huo katika mipango yake ya ufungaji kutizama upya namna ya kuendelea kusaidia jamii kwenye miradi mingine ukiacha miradi ya afya , elimu na miundombinu ila ni muhimu wananchi wanaozunguka mgodi kujengewa uwezo kwenye maeneo ya kilimo.

“Katika hatua za ufungaji ni muhimu kutizama eneo la (social livelihood project) ni muhimu jamii hasa vijana kwenye maeneo ya migodi kujengewa uwezo wa kilimo na wachimbaji wadogo kuwasaidia kwa kusafisha mawe yao kwa namna ambayo ni nafuu zaidi,,” amesema Mhandishi Kamando.

Naye Meneja Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu , Agapith Paul amesema wamechukua maelekezo ya kamati hiyo na watayafanyia kazi kwa maslahi mapana ya nchini na watanzania kwa ujumla.

Aliongeza kuwa mgodi huo utaendelea kuzingatia masuala ya usalama mahali pa afya na utunzaji wa mazingira, alisisitiza kuwa uongozi wa mgodi huo utazingatia mambo yote watakayoelekezwa na kamati hiyo.

Bw. Paul akijibu swali la mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu barabara ya Kahama- Kakola ya kilomita 73 inayojengwa na Migodi ya Barrick nchini , amesema mradi huo wa barabara unajengwa kwa asilimia 100 na mgodi na unasimamiwa na Wakala wa barabara nchini (Tanroads)

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga , CP Salum Rashid Hamduni, amesema uwepo wa migodi ya Barrick kwenye mkoa wa Shinyanga ni fursa ya ajira kwa vijana , zabuni kwa wakandarasi wazawa na ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi ndani ya Mkoa.

Amefafanua serikali ya Mkoa wa Shinyanga itaendelea kushirikiana na mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa sababu ya mchango mkubwa kupitia sera na kanuni za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ambapo kuna ujenzi mkubwa wa mashule maeneo yanayozunguka mgodi na mradi wa kuboresha miundombinu ya elimu nchini nzima , vituo vya afya na uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Kamati ya Kitaifa ya Ufungaji Migodi (NMCC) ilianzishwa rasmi nchini Tanzania kufuatia kuanzishwa kwa Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Na. 15), na kuwekwa kwa miongozo thabiti ya ufungaji migodi iliyozinduliwa rasmi mnamo mwaka 2019.

Jukumu lake kuu ni kupitia na kuidhinisha Mipango ya Ufungaji Migodi (Mine Closure Plans). Hii inasaidia kuhakikisha kuwa mara shughuli za uchimbaji zinapokoma, migodi inafungwa kwa kuzingatia viwango vya usalama, afya, na utunzaji wa mazingira. Pia, kamati inahakikisha maeneo hayo yanarejeshwa katika hali salama ili yaweze kutumika kwa shughuli nyingine za kiuchumi kwa manufaa ya jamii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com