Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BANDARI YA KIGOMA KUFUNGUA FURSA MPYA ZA BIASHARA DRC WAZIRI - MBARAWA



Na Sheila Ahmadi, Kigoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua meli nne mpya za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 2000 kwa safari moja

Hayo yamesemwa Mkoani Kigoma mara baada ya kuzungumza na wanahabari Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema meli hizo ambazo zinatarijiwa kufanya safari zake ndani ya ziwa Tanganyika kutokea Kigoma kuwenda katika nchi za ukanda wa ziwa Tanganyika ikiwemo Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo ( DRC) Burundi ambazo zitakuwa na uwezo wa kubeba tani 832 kwa mwaka.

​“Hatua hii itaufanya mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha usafirishaji na biashara kwa nchi za ukanda wa Ziwa Tanganyika,” alisema Waziri Mbarawa

Aidha Waziri amebainisha kuwa uzinduzi huo utachochea ongezeko la fuesa za kiuchumi ikiwemo kuzalisha ajira mpya za moja kwa moja 600 wakiwemo madereva na wahudumu wa kwenye meli." Amesema Waziri Mbarawa

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kigoma balozi Simon Sirro amesema kuwa, ujio wa meli hizo utatatua changamoto ya usafirishaji wa mizigo kuelekea nchini Congo DRC ambapo awali kulikuwa na ucheleweshaji wa shehena za mizigo kwa takribani miezi miwili.

Vilevile uzinduzi wa meli hizo, Rais Samia ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kipande cha sita kutoka Tabora, kuelekea mkoani Kigoma inayogharimu zaidi ya bilioni mbili.













Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com