Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUENDELEA UBORESHA NA KUJENGA MIUNDOMBINU YA UVUVI






NA MWANDISHI WETU – SONGEA

Serikali inaendelea kuboresha na kujenga Miundombinu ya uvuvi ikiwemo masoko ,maghala ya kuhifadhia mazao ya uvuvi, vichanja vya kukaushia samaki maghala ya kuhifadhia mazao ya uvuvi na viwanda vya kuchakata mazao ya uvuvi na teknolojia rafiki za ukaushaji ili kubadilisha sekta hiyo kutoka ufugaji na ukulima mdogo kuelekea katika kuimarisha lishe na uchumi wa wakulima wadogo wanaojikita katika uzalishaji na ukuzaji wa viumbe maji nchini ambapo matokeo hayo yanatarajia kuchochea uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.



Hayo yameelezwa na Bw. Jumanne Mwankoo Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma wakati wa tukio la kuhakiki taarifa ya matokeo ya mwisho ya mradi wa kuimarisha lishe kwa wakuzaji wadogo wa viumbe maji (ARNSA) uliokuwa ukiratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Uratibu wenye Ulemavu kwa msaada wa Shirika la NORAD kupitia Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo Duniani IFAD tarehe 5 Juni 2026.Bw. Mwankoo alisema kuwa Mradi huo wa kikanda uliokuwa katika Nchi za Tanzania, Kenya na Msumbiji na kutekelezeka katika Mikoa ya Lindi Mtwara na Ruvuma nchini,



Ambao umetoa mchango mkubwa katika sekta ya uvuvi ambayo imechangia takribani asilimia 69% ya protini katika lishe bora, uzalishaji wa mazao ya viumbe maji sambamba na ongezeko la ajira kwa vijana na wanawake na kuimarisha lishe kwa wakuzaji wadogo wa viumbe maji, hususan wakulima wa mwani na wafugaji wa samaki katika Halmashauri za Mtama, Ruangwa Songea na Mbinga



Akiongea wakati wa kufunga mradi huo wa Lishe, Mratibu wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu Bw. Salimu Mwinjaka Alisema kuwa, mradi huo wa miaka miwili ulijikita zaidi katika katika kilimo cha mwani na uzalishaji wa viumbe maji ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani wanufaika wa mdari huo bado wanaendelea na shughuli hizo za uzalishaji kwa kutumia teknolojia za kisasa na ubunifu waliojijengea.








Kwa pande wake Mkurugenzi wa Ukuzaji viumbemaji toka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Nazaeli Madala alieleza kuwa, Serikali imeweka msisistizo katika kukuza uchumi na mikoa iliyotekeleza mradi huo imeweza kukuza uchumi.








‘Mkoa hiyo imebahatika kupata ardhi nzuri na imekuwa fursa ya kuweza kufuga na kupata chakula na kuwauzia wengine chakula, kupata uzalishaji ulio na tija pamoja na uzalishaji Ajira na huu ndo msukomo wa Serikali.” Alibainisha Dkt Madala.
Aidha Aliwaasa wanufaika wa Mradi huo kuwapatia wengine ujuzi walioupata na kuwa waaminifu wanapopata mikopo kupitia Bank ya Kilimo nchini TADB kwa kuirejesha kwa wakati kwa amendeleo ya Taifa.Afisa Uvuvi kutoka Cameroon Bi Audrely Tchoundi aliwapongeza wafugaji wa Tanzani kwa kuwa wabunifu katika eneo la ufungaji viumbemaji na ukulima wa mwani kwa kutumia mbinu mbadala akitolea mfano wakulima wa Mwani wa Kijiji cha Shuka Mkoani Lindi, pamoja na usimamizi mzuri wa mabwawa ya samaki.



Mmoja wa wanufaika wa Mradi huo mwakilishi wa vijana Bw. Innocent Kikiwa Amesema kuwa mradi huo umemuwezesha yeye kama kijana kuweza kupata uzoefu katika eneo la Ufugaji Viumbemaji na kilimo cha mwani, kuweza kujiajiri kukuza mnyororo wa thamani kwa kuuza mazao yatokanayo na zao la mwani, kuuza samaki anaowafuga pamoja na kutafuta masoko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com