Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi leo Mei 21, 2026 amekagua maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa katika Uwanja wa Vita mkoani Tabora.
Akizungumza mara baada ya kukagua maandalizi hayo Dkt. Abbasi amesema maadhimisho hayo yatafanyika Mei 22, 2026 na Mgeni Rasmi katika maonesho hayo ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
Amewataka Wananchi wa Mkoa wa Tabora kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa vita kunakofanyika maonesho hayo ambapo bidhaa na elimu mbalimbali kuhusu nyuki na mazao yake zitaoneshwa.
Awali kabla ya kufanya ukaguzi wa maonesho hayo Dkt. Abbasi akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Emmanuel Buhohela amefanya mahojiano katika studio za Radio Uyui FM na kuzungumza masuala kadhaa kuhusu maandalizi ya Maadhimisho ya kilele cha siku ya nyuki duniani, uhifadhi, utalii na nafasi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuelekea fainali za michuano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON 27) yanayotarajiwa kufanyika katika nchi tatu za Afrika Mashariki Tanzania ikiwemo.










Social Plugin