
Legendary Expeditions, kampuni ya Kitanzania inayoendesha huduma za safari yenye misingi yake katika usimamizi na uwajibikaji wa muda mrefu katika kuhifadhi mifumo ya ikolojia ya Serengeti na Bonde la Ngorongoro, imeingia katika ushirikiano na Auberge Collection chini ya chapa ya Auberge Safari.
Auberge Safari sio upanuzi wa biashara bali ni muunganiko, unaounganisha Legendary Expeditions na Auberge, chini ya utambulisho mmoja.
Ni muunganiko wa chapa mbili zinazojengwa na imani moja iliyoziunda kwamba uzoefu bora zaidi hutokana na mahali penyewe.
Legendary inaleta mandhari ya kipekee ya pori la Afrika Mashariki kwenye mtandao wa Auberge – hii ni Afrika ikitambulishwa kwa hadhira ya kimataifa ya Auberge.

Legendary Expeditions na Auberge Collection zinashirikiana katika maono makuu mawili ambayo ni: ulinzi wa maeneo ya pori na sanaa ya kutoa huduma za ukarimu bora.
Kwa zaidi ya miongo minne, Legendary Expeditions imekuwa mstari wa mbele katika kulinda mazingira ya Tanzania kupitia programu za uhifadhi na maendeleo ya jamii.
Legndary Expeditions ni mfano halisi wa dhamira hiyo.
Auberge Collection ni mshirika wake wa kimataifa anayeshiriki maono hayo ya kuthamini maeneo, utambulisho na ubora wa uzoefu.
Ushirikiano huu unahusisha mali zote sita za Legendary Expeditions: Mwiba Lodge na Mwiba Plains zilizopo katika eneo kubwa la hifadhi ya kipekee kusini mwa Serengeti; Mila, kambi
ndogo ya hema katika Serengeti ya Magharibi; Nyasi na Songa, kambi za hema za mtindo wa zamani karibu na vivuko vya mto Mara; Legendary Lodge, iliyopo Arusha ndani ya shamba la kihistoria la kahawa.
Jambo ambalo ubia huu unaashiria sio upanuzi bali ni muunganiko – maono mawili
yanayofanana sasa yakifanya kazi chini ya utambulisho mmoja.
Legendary Expeditions itaendelea kufanya kazi kama ilivyokuwa awali, ikiwa chini ya timu zilezile, ikiendeshwa kwa viwango vilevile vya uhifadhi, na kuendelea kushikilia misingi yake ya muda mrefu iliyopo.
Uzoefu unabaki kuwa halisi, wa kusisimua na huru na sasa ukiwafikia watu wengi zaidi duniani kote.
Kuhusu Legendary Expeditions
Legendary Expeditions inaendesha moja ya mitandao mikubwa na yenye utofauti wa safari kaskazini mwa Tanzania ndani ya mifumo ya ikolojia ya Serengeti na Ngorongoro.
Mali zake sita, Mwiba Lodge, Mwiba Plains, Mila, Nyasi, Songa na Legendary Lodge zinatoa fursa ya kipekee isiyolinganishwa ya kufikia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na eneo la hifadhi ya wanyamapori la Greater Mwiba.
Kwa kushirikiana na taasisi yake, Friedkin Conservation Fund, Legendary Expeditions
inaunga mkono uhifadhi wa muda mrefu wa maeneo kupitia program za kupambana na ujangili, kulinda makazi ya wanyamapori na uwezeshaji wa jamii zinazozunguka maeneo hayo.
Kuhusu Auberge Collection
Auberge Collection ni mkusanyiko wa hoteli 39 za kipekee, risoti, kambi za safari, nyumba za wageni na vilabu binafsi vilivyoenea katika mabara matatu. Kila eneo lina upekee wake,
lakini yote yanazingatia ubunifu wa hali ya juu, vyakula bora, ustawi wa kisasa, na huduma
ya kiwango cha juu isiyoingiliana na faragha ya mgeni. Auberge inawaalika wageni kutengeneza kumbukumbu zisizosahaulika katika baadhi ya maeneo yanayotamanika Zaidi duniani.
Kwa maelezo zaidi tembelea:
auberge.com/safari
Social Plugin