Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANZANIA, BELARUS ZAIMARISHA USHIRIKIANO WA ELIMU NA UWEKEZAJI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya siku tatu kuanzia 28 hadi 30 ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov ambapo ziara yake imelenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano katika maeneo ya kimkakati baina ya nchi hizo mbili.

***********

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI ya Belarus imeendelea kutoa fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Tanzania, hususan katika fani ya tiba kwa mwaka wa masomo 2026/2027, hatua inayotokana na kuimarika kwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Mbali na hilo, pande hizo mbili zinatarajia kupanua wigo wa ushirikiano huo kwa kujumuisha fani za uhandisi, sayansi ya data na akili bandia, sambamba na kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma na kitaasisi kati ya vyuo vyao vikuu, ikiwemo Sokoine University of Agriculture (SUA) na vyuo vikuu vya Belarus.

Hayo yameelezwa Aprili 28, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya siku tatu ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov, ambayo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano katika maeneo ya kimkakati.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo amesema katika jitihada za kupunguza urasimu unaoweza kuathiri biashara na uwekezaji, ameishauri Belarus kuanzisha ubalozi kamili nchini Tanzania.

“Hatua hii itakuwa chombo muhimu katika kukuza diplomasia ya uchumi na kurahisisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya pamoja kwa ufanisi zaidi,” amesema Balozi Kombo.

Aidha, amesema Tanzania imekaribisha uwekezaji kutoka Belarus katika sekta ya kilimo, hususan katika uunganishaji wa matrekta, uzalishaji wa mbolea na uhamishaji wa teknolojia za kisasa za umwagiliaji ili kuongeza tija na thamani ya mazao.

Katika sekta ya afya, amesema Serikali imepokea kwa mikono miwili nia ya kampuni ya Belpharmprom kushirikiana na Medical Stores Department (MSD) katika uzalishaji na usambazaji wa vifaa tiba, hatua itakayoboreshwa upatikanaji wa huduma bora za afya nchini.

Kwa upande wa nishati, Kombo amesema Belarus imealikwa kushiriki kikamilifu katika uwekezaji na utoaji wa huduma za kihandisi, hususan katika maendeleo ya mafuta na gesi, pamoja na miradi ya nishati jadidifu ikiwemo jua, upepo na maji.

Ameongeza kuwa katika sekta ya utalii, idadi ya watalii kutoka Belarus wanaotembelea Tanzania imeongezeka hadi kufikia zaidi ya 6,000 katika miaka ya hivi karibuni, huku juhudi zikiendelea za kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kati ya nchi hizo mbili ili kuchochea zaidi sekta hiyo.

Majadiliano kati ya mawaziri hao yameonesha kuwa Tanzania na Belarus ni mataifa rafiki yenye maono ya pamoja ya maendeleo na ustawi wa wananchi wake.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov amesema Belarus ina dhamira ya dhati ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo, akisisitiza kuwa elimu itaendelea kuwa kipaumbele katika ushirikiano huo.

Ameongeza kuwa nchi yake ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza sekta ya viwanda kupitia uhamishaji wa teknolojia na utaalamu wa kisasa ili kuongeza thamani ya mazao na kuimarisha ushindani wa bidhaa katika soko la kimataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya siku tatu kuanzia 28 hadi 30 ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov ambapo ziara yake imelenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano katika maeneo ya kimkakati baina ya nchi hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya siku tatu kuanzia 28 hadi 30 ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov ambapo ziara yake imelenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano katika maeneo ya kimkakati baina ya nchi hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 28, 2026 Jijini Dar es Salaam kuhusu ziara yake ya siku tatu kuanzia 28 hadi 30 ambayo imelenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano katika maeneo ya kimkakati baina ya nchi hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov ambaye amewasili nchini kwaajili ya ziara yake ya siku tatu ambapo ziara yake imelenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano katika maeneo ya kimkakati baina ya nchi hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov ambaye amewasili nchini kwaajili ya ziara yake ya siku tatu ambapo ziara yake imelenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano katika maeneo ya kimkakati baina ya nchi hizo mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov ambaye amewasili nchini kwaajili ya ziara yake ya siku tatu ambapo ziara yake imelenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano katika maeneo ya kimkakati baina ya nchi hizo mbili.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com