Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAMA LISHE USO KWA USO NA RAIS SAMIA - WATAKA AMANI



Na mwandishi wetu, Dar

Mwenyekiti wa umoja wa mama na baba lishe Tanzania (UMALITA), Havijawa Omary, ametoa wito kwa watanzania kusimama imara katika kulinda amani na utulivu wa taifa. Akiwahimiza kuepuka kurubuniwa na maneno ya uchochezi au migogoro ya kisiasa.

Havijawa ameyasema haya Leo April 20, 2026 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kongamano kubwa la mama na baba lishe linalotarajiwa kufanyika jijini hapa ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa ni Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan

"Uza chakula chako, uzia wateja wako, na sambaza amani," alisisitiza Havijawa, akibainisha kuwa utulivu ndio msingi pekee utakaowezesha mama na baba lishe kutimiza ndoto zao na kunufaika na fursa za mikopo na nishati safi.

Amesema wana imani na Rais Samia kwamba anakwenda kuwafungulia fursa za Mikopo na kuifanya kazi hiyo ya kuwahudumia watanzania chakula ionekane ina thamani, kwani kupitia kazi hiyo wengine wameweza kujenga na kusomesha watoto.

Aidha ametoa wito kwa Mama na Baba lishe kote nchini kujitokeza kwa wingi kwenye kongamano hilo ili waweze kumsikiliza na kupokea maelekezo kutoka kwa Rais Samia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com