
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, amekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe kutoka Kampuni ya Datavera, wataalam wa mifumo ya kidijitali.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Aprili 15, 2026, Bungeni Jijini Dodoma, yakihusisha pia wataalam wa wizara.
Katika kikao hicho, Waziri Makonda amepokea wasilisho kuhusu suluhisho za mifumo ya kidijitali zitakazosaidia kuimarisha ufanisi na maendeleo ya sekta zilizo chini ya wizara hiyo.
Hatua hii inaonesha mwelekeo wa Serikali katika kutumia teknolojia kuboresha utendaji, uwazi na utoaji wa huduma kwa wananchi.




















Social Plugin