Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAJI CHANDE NI MWANDAMIZI NA MWISHO WA PROPAGANDA ZA KITOTO

Leo tarehe 23 Aprili, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman anakabidhi ripoti inayokwenda kuzika rasmi upotoshaji kuhusu matukio ya Oktoba 29,2025. 

Jaji Chande siyo mtu wa kuyumbishwa ni nguli mwenye uzoefu wa kimataifa aliyebobea kwenye uchunguzi na sheria za haki za binadamu. 

Anakuja na ukweli wa kitaalamu, siyo ramli za mitandaoni.

Tume yake imefanya kazi kwa uhuru na weledi wa hali ya juu. 

Ripoti hii inakuja kumaliza utata uliokuwepo kuumbua wapotoshaji na kuliunganisha taifa letu. 

Wale waliozoea kupandikiza chuki na kutengeneza simulizi za uongo kwa ajili ya kiki za kisiasa leo ndiyo mwisho wenu.

Jaji Chande hapokei ngano za vijiweni anatoa ukweli mchungu uliothibitika kisheria. 

Watanzania tuwe watulivu ukweli unaenda kuwekwa hadharani na kuliweka taifa huru dhidi ya propaganda za kilaghai

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com