Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Buduhe, kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, limefanya mkutano wake uliojadili ajenda mbalimbali kuhusu uhai na maendeleo ya chama hicho.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Aprili 27, 2026, Mwenyekiti wa tawi hilo, Joseph Yakanda, amesema kuwa uhai wa chama unatokana na uwepo wa vikao vya mara kwa mara vinavyowezesha kufanya tathmini ya shughuli mbalimbali kwa umoja na mshikamano.
“Wanachama wenzangu, tunapokutana hapa tunapata fursa ya kujadiliana na kushirikishana mawazo kwa pamoja ili kufikia maamuzi ya pamoja, ambayo baadaye tunayatekeleza kwa lengo la kukifanya chama chetu kuendelea kukua na kuvutia wananchi wengine kujiunga nasi,” amesema Yakanda.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Buduhe Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Joseph Yakanda akizungumza kwenye kikao cha tawi hilo kuhusu uhai wa Chama Aprili 27, 2026
Kwa upande wake, Katibu wa tawi hilo, Mahembo Ndamo, amezungumzia umuhimu wa wanachama kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama pamoja na kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha uhai wa chama.
Naye Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira, Godfrey Nyalulu, amepongeza wanachama huku akieleza kuwa hali hiyo ndiyo chachu ya mafanikio na ukuaji wa chama.
Aidha, Mlezi wa tawi hilo, Francisca Bahame, amewakumbusha wanachama umuhimu wa kuwa wazalendo kwa chama hicho pamoja na kufuata maadili na miongozo wanayopewa na viongozi wao.
Mkutano huo umewakutanisha wanachama wa tawi hilo kujadili masuala mbalimbali ya chama na kuweka mikakati ya kuimarisha uhai wake kupitia umoja na mshikamano.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Buduhe Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mahembo Ndamo akizungumza kwenye kikao cha tawi hilo kuhusu uhai wa Chama Aprili 27, 2026
Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Buduhe Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shiinyanga Francisca Bahame akizungumza kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) tawi la Buduhe Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mwantumu Zumo akiwa kwenye kikao Cha kujadili uhai wa Chama hicho Aprili 27, 2026
Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira (CCM) tawi la Buduhe Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Godfrey Nyalulu akizungumza kwenye kikao cha tawi hilo kuhusu uhai wa Chama Aprili 27, 2026
Social Plugin