Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi, akizungumza katika Mahafali ya 14 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Mwendakulima, Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.

Naibu Meya wa Manispaa ya Kahama na Diwani wa Kata ya Mwendakulima, Shabani Mikongoti, akizungumza katika Mahafali ya 14 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Mwendakulima, Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwendakulima, Bi. Neema Mfumya, akizungumza katika Mahafali ya 14 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Mwendakulima, yaliyofanyika Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwendakulima, Bi. Neema Mfumya, akizungumza katika Mahafali ya 14 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Mwendakulima, yaliyofanyika Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.
Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi, akigawa vyeti kwa wahitimu katika Mahafali ya 14 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Mwendakulima, yaliyofanyika Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.

Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi, akiwa katika Mahafali ya 14 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Mwendakulima, yaliyofanyika Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.
Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi, akigawa vyeti kwa wahitimu katika Mahafali ya 14 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Mwendakulima, yaliyofanyika Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.
Wahitimu wakiwa katika Mahafali ya 14 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Mwendakulima, Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.
***
Kampuni ya Barrick nchini yenye ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora katika mazingira salama na rafiki kwa kujifunzia.
Katika kuendeleza dhamira hiyo imetoa msaada wa mifuko 100 ya saruji, ndoo 10 za rangi pamoja na malori mawili ya mchanga kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa na uzio wa Shule ya Sekondari Mwendakulima, iliyopo Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.
Akizungumza wakati wa mahafali ya 14 ya kidato cha sita ya shule hiyo, Meneja wa Ufungaji wa Mgodi wa Barrick Buzwagi, Mhandisi Zonnastral Mumbi ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema Barrick itaendelea kushirikiana na jamii katika kuboresha sekta ya elimu.
"Elimu ni moja ya sekta ambayo kampuni ya Barrick inaipa kipaumbele kikubwa ambapo tumefanikisha miradi mbalimbali ya elimu mkoani Shinyanga na nchini kwa ujumla pia tunazo programu za kunufaisha wanafunzi wa kitanzania", alisema Mhandisi Mumbi.
Awali, akisoma risala kwa niaba ya wahitimu, Agnes Julius alisema licha ya shule hiyo kufanya vizuri kitaaluma, bado inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa vyumba 10 vya madarasa pamoja na ukosefu wa uzio, hali inayohatarisha usalama wa wanafunzi wanaoishi shuleni hapo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule, Bi. Neema Mfumya, aliipongeza kampuni ya Barrick kwa ushirikiano wake wa muda mrefu katika kuisaidia shule hiyo.
Naye Naibu Meya wa Manispaa ya Kahama, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mwendakulima, Shabani Mikongoti, aliwasisitiza wazazi kuwa karibu na watoto wao, hususan wanapokuwa masomoni.
"Nawapongeza wahitimu wote na natoa rai kwenu muendelee kupambana kwa kuwa katika maisha kunahitajika kufanya kazi kwa bidii katika suala lolote mtakalofanya pia kuzingatia kuwa na nidhamu",alisisitiza.

Social Plugin