Meneja wa Kanda ya Kaskazini (TBS), Mhandisi Ismail Mwaipaja, akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Arusha kuhusu mafanikio na utekelezaji wa majukumu ya kanda hiyo
Mhandisi Mwaipaja amesema TBS Kanda ya Kaskazini imefanikiwa kuthibitisha ubora wa bidhaa za wazalishaji pamoja na wajasiriamali 492, ambapo kati yao 238 ni wajasiriamali wadogo. Hatua hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi na kuhakikisha soko linakuwa na bidhaa bora na salama kwa watumiaji.
Aidha, ameeleza kuwa TBS inaendelea kuboresha huduma na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zake, ikiwa ni pamoja na mpango wa kujenga maabara mpya jijini Arusha ili kurahisisha upimaji na uthibitishaji wa ubora wa bidhaa.
Vilevile, TBS inaendelea kutoa mchango katika kuhakikisha ubora wa vifaa vinavyotumika katika miradi mikubwa ya maendeleo nchini, ikiwemo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya michezo inayohusiana na maandalizi ya michuano ya Africa Cup of Nations (AFCON), kwa kuhakikisha vifaa vya ujenzi vinakidhi viwango vinavyotakiwa.



Social Plugin