Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James akizungumza wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Habari/Wahariri na Waandishi wa Habari 2026 (MISA TAN SUMMIT' lililoandaliwa na MISA Tanzania. Picha na Kadama Malunde
Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko akizungumza kwenye Kongamano la Wadau wa Habari/Wahariri na Waandishi wa Habari 2026 (MISA TAN SUMMIT' lililoandaliwa na MISA Tanzania.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, amesema uwepo wa wahariri na waandishi wa habari kutoka maeneo mbalimbali ya nchi unaonesha umuhimu mkubwa wa sekta ya habari katika kujenga taifa lenye uwazi, uwajibikaji na maendeleo endelevu, huku akisisitiza kuwa vyombo vya habari vina jukumu la msingi la kuhabarisha, kuelimisha na kuchochea mjadala wa maendeleo katika jamii.
Kauli hiyo ameitoa leo Machi 17, 2026 wakati akifungua rasmi Kongamano la Wadau wa Habari/Wahariri na Waandishi wa Habari 2026 (MISA TAN SUMMIT' lililoandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (Media Institute of Southern Africa - MISA), tawi la Tanzania (MISA Tanzania) lililofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa likiongozwa na kauli mbiu 'Iringa Imara Tutaijenga kwa Umoja na Uwajibikaji'.
Amesema uwepo wa wadau hao wa habari ni muhimu katika kuimarisha misingi ya uwazi na uwajibikaji katika jamii, akibainisha kuwa sekta ya habari ina nafasi kubwa katika kuathiri fikra na mwelekeo wa maendeleo ya taifa.
Mhe. James ametumia fursa hiyo kuwakaribisha washiriki wote mkoani Iringa, akieleza kuwa mkoa huo una mazingira rafiki ya uwekezaji na rasilimali nyingi zikiwemo kilimo, mifugo, misitu na utalii, huku akisisitiza kuwa uchumi wake unaendelea kukua kwa kasi.
Aidha, amesema Serikali imeendelea kuwekeza katika miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo afya, elimu, miundombinu ya barabara, maji, nishati na utalii, hali inayochochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. Amebainisha kuwa sekta ya kilimo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa mkoa huo.
Katika sekta ya utalii, amesema Mkoa wa Iringa una vivutio muhimu kama Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Udzungwa pamoja na maeneo ya kihistoria kama Kalenga, na kuutaja kuwa kitovu cha utalii katika ukanda wa kusini mwa Tanzania.
Kwa upande wa miundombinu, amesema Serikali imeendelea kuboresha barabara, huduma za umeme na maji pamoja na usafiri wa anga kupitia uboreshaji wa Uwanja wa Ndege wa Nduli ili kufungua fursa zaidi za biashara na uwekezaji.
Amewataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuitangaza Iringa na Tanzania kwa ujumla ili kuvutia wawekezaji na watalii pamoja na kuchochea maendeleo ya taifa.
Pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za Serikali yake katika kuleta miradi ya maendeleo inayochangia ustawi wa wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa MISA Tanzania, Edwin Soko, amesema kongamano hilo linalenga kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na wadau wa maendeleo, sambamba na kukuza uandishi wa habari unaotoa suluhisho kwa changamoto zinazoikabili jamii.
Amesisitiza kuwa taasisi hiyo itaendelea kulinda uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza na haki ya kupata taarifa, huku akiwahimiza waandishi wa habari kuzingatia weledi na maadili ya taaluma katika kuandika habari zenye mwelekeo wa kutatua matatizo ya wananchi.
Aidha, Soko ameeleza kuwa, kufuatia kuvutiwa na mazingira na fursa zilizopo mkoani Iringa, MISA Tanzania ina mpango wa kuanzisha kituo maalum cha mawasiliano na ugawaji wa taarifa za maendeleo kitakachohudumia pia mikoa jirani. Kutokana na hilo, ameomba Serikali ya Mkoa wa Iringa kutoa eneo la ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho.
Akijibu ombi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, ameagiza uongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuanza mara moja mchakato wa kutafuta na kutenga eneo la ardhi kwa ajili ya MISA, akieleza kuwa mkoa huo umefarijika kupokea ugeni mkubwa wa wadau wa habari na uko tayari kuunga mkono juhudi hizo.
“Naomba RAS pamoja na wakuu wa idara muanze mchakato wa upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya wenzetu wa MISA, hatua ambayo pia itakuwa chachu ya taasisi hiyo kuendelea kurejea Iringa,” amesema Kheri James.
Ameongeza kuwa ushirikiano huo ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Mkoa katika kuimarisha sekta ya habari na kuhakikisha Iringa inanufaika na uwepo wa taasisi hiyo, hususan katika utoaji wa taarifa za maendeleo na fursa kwa wananchi wa ndani na maeneo jirani.
Katika hatua nyingine, Meneja wa National Social Security Fund (NSSF) Mkoa wa Iringa, Benedict Wela, amesema taasisi hiyo inaendelea kutoa elimu na kuwahamasisha Watanzania kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kujikinga na changamoto za kiuchumi na kuwa na uhakika wa kipato baada ya kustaafu.
Kongamano hilo limewakutanisha waandishi wa habari, wahariri, viongozi wa serikali pamoja na wadau mbalimbali, likiwa na lengo la kujadili mchango wa sekta ya habari katika kuchochea maendeleo ya Mkoa wa Iringa na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James akizungumza wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Habari/Wahariri na Waandishi wa Habari 2026 (MISA TAN SUMMIT' lililoandaliwa na MISA Tanzania. Picha na Kadama Malunde
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James akizungumza wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Habari/Wahariri na Waandishi wa Habari 2026 (MISA TAN SUMMIT' lililoandaliwa na MISA Tanzania. 

Social Plugin