SERIKALI YALENGA MAPINDUZI YA NISHATI SAFI NCHINI WAZIRI GWAJIMA
Na Mwandishi Wetu Dar es salaam
Serikali imelenga Mapinduzi ya nishati safi nchini huku zaidi ya kaya bado zikitumia kuni na mkaa kama nishati kuu ya kupikia, ambapo takwimu mpya za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (Sensa ya Watu na Makazi 2022) zimebainisha.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, asilimia 55.5 ya kaya hutumia kuni huku asilimia 26 zikitumia mkaa, hali inayotajwa kuendelea kuchangia madhara ya kiafya na uharibifu wa mazingira. Ni asilimia 18.5 pekee ya kaya zinazotumia nishati safi, ambapo asilimia 9.4 hutumia gesi, asilimia 4.3 umeme na asilimia 4.6 vyanzo vingine mbadala.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe Dorothy Gwajima kwenye kongamano lilioandaliwa wanawake wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO ambapo amesema kiwango cha matumizi ya nishati safi nchini bado ni Hafifu ukilinganisha na athari zinazotokana na matumizi ya kuni na mkaa.
“Asilimia 18.5 ni ndogo kwa taifa linalolenga maendeleo endelevu. Tunahitaji mapinduzi ya pamoja ya kimtazamo na kiteknolojia ili kuwalinda wanawake na watoto ambao ndio waathirika wakubwa wa moshi wa kupikia,” alisema Dkt. Gwajima.
Aidha moshi utokanao na nishati zisizo safi huchangia magonjwa ya mfumo wa hewa na kuongeza mzigo wa kiafya kwa familia nyingi.
Kwa upande wake, uongozi wa TANESCO ulisema shirika hilo linaendelea kuboresha miundombinu ya umeme ili kuwezesha wananchi wengi zaidi kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi.
“Tutaendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kutoa elimu kwa jamii kuhusu faida za nishati safi. Wanawake ni nguzo muhimu katika kufanikisha mabadiliko haya,” ilieleza sehemu ya taarifa ya shirika hilo.
Vilevile Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeweka ajenda ya nishati safi ya kupikia kuwa kipaumbele cha kitaifa. Kupitia Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na TANESCO na wadau mbalimbali, utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024–2034 unaendelea.
Mkakati huo unalenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034 — hatua inayotarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa kuni na mkaa pamoja na kulinda afya na mazingira.
baby, maybe. We'll turn on camera account mido, the pictures of honey. Pick up the names of caribou. Adaptive changes, oh my God. YouTube on Vietnamese. My mom was Jackie. What's the summer and Jason? The chief of college.






Social Plugin