Na Barnabas Kisengi Dodoma
Leo february 16. 2026 Meneja wa wakala wa barabara za Mjini na vijijini Tarura Mhandisi Emanuel Mfinanga afanya ukaguzi wa miundombinu za barabara za mtaa wa chinyoyo na kujionea jinsi miundombinu hiyo ilivyo haribika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Katika ukaguzi huo wa miundombinu hiyo aliongozana na wataalamu kutoka ofisini kwake na kukutana na Diwani wa kata ya kilimani Mussa Mkunda na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Chinyoyo Faustina Bendera ambao wamemtembeza katika barabara za mtaa huo.
Awali Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Chinyoyo Bendera amemweleza meneja huyo swala la ubovu wa miundombinu ya barabara za mtaa wake zimekuwa kero ya muda mrefu na hazijapata suluhisho kwa muda mrefu jambo ambalo hupelekea wananchi wa mtaa huo kushindwa kutumia barabara hizo.
"Hizi barabara zimekuwa kero kubwa sana kwa wananchi wangu hasa kipindi cha masika huku ukiwa na mgonjwa au mama mjamzito huwezi kumpakia kwenye gari kwakuwa hakupitiki hivyo lazima tumbebe kwenye machela au bodaboda hadi kumfukisha barabarani" amesema Faustina
Kwa upande wake Diwani wa kata ya kilimani Mkunda amesema katika mitaa inayomkosesha usingizi hasa kwa swala la miundombinu ya barabara ni Mtaa wa Chinyoyo ambao hadi Sasa hatujapatiwa tiba ya barabara za mtaa huo.
"Mimi tangu mtoto nimeona hadi sasa nimekuwa mtu mzima na baada ya kurasimishiwa makazi hali ya miundombinu ya barabara za mtaa huu kwakweli hazirizishi kabisa hasa katika kipindi cha masika tumekuwa tunapata tabu sana hivyo meneja tuangalieni kwa jicho la tatu maana unapo taja kata ya kilimani ni kata kubwa yenye viongozi wengi wakubwa lakini miundombinu ya barabara za mtaa wa chinyoyo kwakweli haziridhishi kabisa"amesisitiza Mkunda
Meneja wa wakala wa barabara za Mjini na vijijini Tarura Mhandisi Emanuel Mfinanga amesema kuwa kutokana na hali ya changamoto ya miundombinu ya barabara za mtaa huo atahakikisha anazichukulia uharaka wa kuweka vifusi ili kuhaki wanarekebisha miundombinu hiyo ya barabara ili kuwanusuru wakazi wa mtaa huo.
"Niwaambie Mhe Diwani na Mwenyekiti wa mtaa kweli tumezikagua barabara hizi zote na tumeona hali ya uharibifu mkubwa niwaahidi kuwa tumelichukulia jambo hili kwa ukubwa wake hivyo niwaahidi kuwa kwakuwa serikali ni sikivu hili jambo tumelichukuwa umakini mkubwa hivyo tunakwenda kulifanyia kazi"amesema Mhandisi Mfinanga
Ukaguzi huu wa barabara za mtaa wa chinyoyo ni hukumu letu kama tarura kuhakikisha miundombinu ya barabara zote za kata 41 za Jiji la Dodoma zinafikika kwa urahisi naewananchi wanapita kwa urahisi na kupita na kupata huduma.
Ziara hiyo ya meneja wa tarula na wataalamu imeleta matumaini kwa wananchi wa mtaa wa chinyoyo ambao bado wanasubiri matumaini ya kuona miundombinu hiyo ya barabara ikirekebishwa.

Social Plugin