Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SEGULE AWAONYA WANAOCHUKUA MAJI CHINI YA ARDHI NA JUU YA ARDHI BILA KIBALI



Na Oscar Assenga,MUHEZA

MKURUGENZI Bonde la Maji la Pangani Segule Segule amewaonya watu ambao wanao kuchukua maji chini ya ardhi,juu ya ardhi bila kufuata utaratibu uliowekwa kisheria ikiwemo kuwa vibali kuacha mara moja kwani wakiwafikia watawakamata.

Segule aliyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maji Mto Zigi uliofanyika mjini Muheza ambapo alisema iwe mtu binafasi au taasisi huku akiwashauri wafuate utaratibu na kuchukua vibali na vibali vyao vinawaeleza kitu gani wanapaswa kufanya.

Aliwaeleza wadau wa Jumuiya hiyo kuwa Bonde la Mto Pangani linasimamia vyanzo vilivyopo chini ya ardhi kupitia visima na katika eneo hilo watu wengi hawana ufahamu au wengine wanaelewa lakini hawafuati utaratibu uliowekwa

Aidha alisema watu hawana ufahamu wa kutosha katika eneo la visima kwamba ukipewa ridhaa na Mkurugenzi wa Halmshauri ukipewa hatia na Wizara ya Ardhi juu ya kutumia ardhi na unaporaka kutumia rasilimali maji lazima upate kibali kutoka kwenye Bonde husika na katika Kanda ya Kaskazini anayetaka kutimia maji kutoka chini ya ardhi lazima apate kibali kuyoka Bonde la Pangani.

Aidha alisema kwamba Serikali imefanya kwa nia njema na sio kuweka ugumu watu wasitumie lakini wasiposimamiana katika hilo ipo siku maji yote yatachafuliwa na yanaweza yasiwepo.

Alieleza kwamba wao hawatoi vibali pekee bali wanaratibu wachimbaji kujua wana utaalamu wa kutosha wanaanza kuratibu kwenye utafiti huyo anayefanya utafiti je ana taaluma hiyo mpaka wanapotoa kibali cha kuchimbiwa visima wanauhakika wanakuwa ni watu sahihi wanaotumia utaalamu sahihi hivyo uchimbahji wake hauwezi kuleta madhara kwenye jmii husika,

Awali akizungumza wakati akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Muheza, Katibu Tawala wa wilaya hiyo serikali inatambua ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika usimamizi na uhifadhi na uendelezaji wa rasimali za maji na mazingira.

Alisema lengo kuu katika juhudi hizo ni kuhakikisha rasilimali za maji zinazopatikana kwa wingi ikiwemo ubora unaokubalika na kwa uendelevu wa matumizi ya maji kwa sasa na vizazi vijavyo.

“Niwapongeze viongozi mliomaliza muda wenu kwa kazi nzuri na kubwa mlioifanya na kusimamia uendeshaji wa jumuiya ikiwemo usimamizi wa vyanzo vya maji”Alisema

Aliongeza kwa athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na hali ya hewa hapa nchini ikiwemo Muheza joto kali mvua hazinyeshi hayo yote yamebadilika kutokana na uharibifu wa mazingira unaoendelea.

Alisisitiza utunzaji wa mazingira ni jambo muhimu ambalo limeendelewa kupewa kipaumbele na Rais na hata alipoazimisha siku ya kuzaliwa alipanda miti hivyo kupitia jumuya hiyo waendelee kuwahamasisha watu wapande miti katika kila sikukuu zao muhimu ikiwemo kuzaliwa.

Hata hivyo alieleza kwamba kuna umuhimu wa Jumuiya hizo kuendelea kujengewa uwezo ili kuweza kutunza mazingira ikiwemo mafunzo ya mara kwa mara ili waweze kuendana na kazi na mazingira kipindi cha sasa.











Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com