Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru J. Maghembe (Mb.), amefanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini, Mhe. Yordenis Despaigne Vera, katika Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar Es Salaam tarehe 10 Februari, 2026.
Mazungumzo hayo yamefanyika ili kujadiliana namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Cuba. Tanzania na Cuba zimekuwa na uhusiano wa karibu na kindugu zaidi ya miongo sita iliyopita.
Uhusiano wetu umejengwa tangu enzi za kupigania uhuru ambapo viongozi waasisi wa mataifa yetu, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Hayati Fidel Castro wa Cuba, ambao walijenga msingi wa uhusiano, usawa na maendeleo ya pamoja.
Kwa pamoja viongozi hao, wamejadiliana namna bora ya kuendeleza ushirikiano wa uwili na kimataifa kwa maslahi ya pande zote mbili.
Tanzania na Cuba zilianzisha ushirikiano wa kidiplomasia mwaka 1962.


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)


Social Plugin