Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMANI NDIO MSINGI WA BIASHARA ZETU- MWINYIMVUA



Na mwandishi wetu, Dar

Utulivu na amani vimetajwa kama misingi muhimu katika kuwezesha maendeleo na ustawi wa jamii kiuchumi, msisitizo na tahadhari ikitolewa kwa Watanzania kuhakikisha amani hiyo inasalia nchini, amesema Bi. Mosi Mwinyimvua, Mkazi wa Mvuti Mkoani Dar Es Salaam.

"Amani ni kila kitu kwetu na kama unavyojua sisi akinamama wajasiriamali lazima tutoke tukapate riziki, tunasomesha, tunalea watoto na wengine tumeachiwa watoto bila baba zao sasa bila kutoka kujishughulisha watoto wetu wataishi vipi? Amani ni muhimu."amekaririwa Bi Mwinyimvua.

Mwananchi huyo mjasiriamali akizungumza nasi mapema leo Jumatano Februari 11, 2026, amesisitiza kwamba shughuli za kiuchumi na kijamii bila ya amani huathirika na kuleta hofu kwa jamii, akisisitiza umuhimu wa kila Mtanzania kushiriki katika kulinda na kudumisha amani.

Hali ya amani kulingana na maandiko mbalimbali inatajwa kuwezesha maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kwa kuwa inawapa watu uhuru wa kufanya shughuli zao za kila siku bila wasiwasi na hivyo kutajwa kama msingi wa mafanikio ya jamii yoyote, faida zake zikidhihirika katika kila nyanja ya maisha ya binadamu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com