Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATUMISHI WA WASHIRIKA LA MASOKO WAJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA E-MREJESHO.


Shirika la Masoko ya Kariakoo limeimarisha mfumo wa kupata mrejesho kutoka kwa wateja wake kwa kujiunga katika mfumo e-mrejesho ili kupata mrejesho kwa watu wengi zaidi, kushughulikia na kurudisha mrejesho kwa kwa wananchi kwa wakati na hivyo kuendelea kukuza dhana ya utawala bora katika shirika hilo.

Akifungua mafunzo hayo, Meneja Mkuu wa Shirika hilo CPA. Ashraph Abdulkarim amesema shirika hilo limeshughulikia malalamiko ya wafanyabiashara wa Kariakoo kwa wakati na limeendelea kumpata mrejesho kila wakati kutoka kwa wafanyabiashara wake na wadau wengine.

“Baada ya kuwapangia maeneo wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo, yapo malalamiko yaliibuka lakini tuliwasikiliza kila mmoja na baadae tulipata majawabu kwa pamoja, sasa tunataka kuwa na mfumo ambapo hata mtu akiwa nyumbani kwake anatupa mrejesho kuhusu huduma zetu na tutashugulikia na kumpa mteja mrejesho kwa wakati” amebainisha CPA. Abdulkarim

CPA. Abdulkarim ameongeza kuwa shirika limeteua afisa maalum ambaye atakuwa na jukumu la kuingia kwenye mfumo ili kujua mambo mbalimbali yaliyoibuliwa na wananchi, kuyawasilisha sehemu husika, kufuatilia mrejesho na kuuwasilisha kwa wananchi kwa wakati kwa kuzingatia mkataba wa huduma kwa mteja.

Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo bw. Faraja Mpande amesema kuwa mfumo wa e-mrejesho ni miungoni mwa mifumo bora duniani na umeshinda tuzo mbalimbali kwa namna ya kushughulikia mrejesho wa wananchi kwa wakati na kuwahamasisha wananchi kuutumia mfumo ipasavyo kuwasiliana na serikali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com