Na Sumai Salum-Kishapu
Kamati ya Kudumu ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo yenye zaidi ya Tsh. Bil. 1.2.
Ziara hiyo iliyohusisha baadhi ya Madiwani na Menejimenti imefanyika mnamo Januari,14-15, 2026 Kata ya Kishapu,Lagana,Talaga,Maganzo,Songwa,Mondo na Sekebugoro huku ikikagua jumla ya miradi tisa.
Tazama picha za miradi mbalimbali
Ujenzi wa Madarasa 2 ya Awali na Matundu 6 ya Choo – Shule ya Msingi Isoso wenye thamani ya Tsh 71,800,000 chanzo cha fedha ni mradi wa Boost





Ujenzi wa Kituo cha Afya Lagana (OPD na Maabara) wenye thamani ya Tsh 250,000,000 chanzo cha fedha ni kutoka serikali kuu


Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Matundu 6 ya Choo – Shule ya Msingi Nhobola wenye thamani ya Tsh 66,200,000 chanzo cha fedha ni mradi wa Boost
Ujenzi wa Vizimba 200 – Soko la Maganzo mradi unaotekelezwa kwa fedha za CSR ya Mgodi wa Almas Mwadui WDL wenye thamani ya Tsh 260,000,000Ujenzi wa Matundu 5 ya Choo –soko la Maganzo fedha za CSR kutoka Mgodi wa Almas Mwadui WDL wenye thamani ya Tsh 20,000,000
Ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Songwa kwa fedha za CSR kutoka Mgodi wa Almas Mwadui ( WDL) wenye thamani ya Tsh 47,000,000
Ujenzi wa Zahanati ya Seke Ididi wenye thamani ya Tsh 101,989,971 chanzo cha fedha kikiwa ni CSR kutoka kampuni ya ujenzi ya CCECC













Social Plugin