Na mwandishi wetu,Dar
Kuelekea siku 100 za awali za uongozi wa kipindi cha Pili cha Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mzee Bosco Nchimbi, Mkazi wa Dar Es Salaam ameonesha kuridhishwa na kazi nzuri ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na serikali ya Rais Samia.
Mzee Nchimbi amebainisha hayo leo Jumatano Januari 28, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari Temeke, Jijini Dar Es Salaam, akisema amebahatika kuwepo katika awamu zote za serikali, na kulinganisha na awamu zilizopita, Rais Samia amefanya kazi kubwa katika kuboresha na kusimamia utoaji wa huduma za kijamii na usimamizi katika miradi ya maendeleo kote nchini.
"Mimi kwa upande wa mama sina deni nae,amefanya mengi yanayoonekana kwa macho na hata wanaobeza uongozi wa Mama ninaamini huyo akili zake si nzuri. Angalia kuanzia kwenye barabara na kadhalika."
"Ndio maana wanasema nani kama Mama? Nyumba yoyote ikiwa imetulia ujue sifa ni kwa mama na hakika mama anatulea, sina deni nae. Kwakweli anajitahidi sana na ni muhimu kukumbuka kuwa mti wenye matunda ndio hupigwa mawe kwahiyo Mama naomba awavumilie tu " ameongeza kusema Bw. Nchimbi.

Social Plugin