Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATUMISHI WA MAENDELEO YA JAMII TUWAJIBIKE – MHE.MARYPRISCA



Na Jackline Minja WMJJWM- Dodoma.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka watumishi wa Kituo cha Huduma kwa wateja kuwajibika kwa kuwahudumia wananchi na kutatua changamoto zao.

Mhe. Maryprisca ameyasema hayo leo tarehe 10 Desemba, 2025 alipotembelea kituo hicho ikiwa ni ziara ya kujifunza namna kinavyowahudumia wananchi.

Akizungumza mara baada ya kusikiliza maelezo ya watumishi hao, Naibu Waziri Maryprisca amekiri kuwa kituo hicho kinafanya kazi kubwa na yenye mchango mkubwa katika kuboresha utoaji wa taarifa na huduma kwa umma.

Aidha Mhe. Maryprisca ameahidi kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa majukumu katika ngazi zote, ikiwemo kutoa maelekezo mahsusi kwa halmashauri na idara zinazohusika ili kuhakikisha taarifa kutoka katika kituo cha huduma kwa wateja zinashughulikiwa kwa wakati na kuimarishwa kwa utoaji wa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya Wizara na namna ya kutoa malalamiko ili kupunguza mkanganyiko unaojitokeza.

Ziara hiyo ya Naibu Waziri Maryprisca inalenga kuboresha mifumo ya uwajibikaji, kuongeza ufanisi wa huduma na kuhakikisha sauti za wananchi zinapokelewa na kufanyiwa kazi kwa uharaka na weledi unaostahili.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com