
Richard Lukweli, mkazi wa Morogoro, ametoa wito kwa Watanzania kulinda Taifa kwa kuweka msingi wa upendo na amani. "Watanzania tuiilinde Taifa letu kwa kuweka msingi wa upendo, amani umoja na mshikamano ili Taifa liweze kuendelea kwa kasi," alisema. Alionya kuwa maendeleo hayawezi kupatikana kama hakutakuwa na amani.
Naye Salum Ally, Katibu wa Shirika la Taasisi ya Kudumisha na Kuona (TLB) mkoani Morogoro, alisisitiza kuwa Tanzania lazima iendelee kufurahia amani iliyopo na kukataa chokochoko. "Tunatamani amani iliyopo Tanzania tuzidi kuifurahia na kukataa chokochoko zozote zinazotaka kuchafua amani. Hakuna Tanzania nyingine ambayo tutakaa," alieleza, akiongeza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda amani.
Kwa upande wa wanawake, Jamila Maftu, mkazi wa Morogoro, alikemea vikali wale wote wanaochochea vurugu na kutaka kuangusha Serikali. "Kina mama tusiruhusu chokochoko zozote za kutaka kuangamiza Taifa letu," alisema. Alisema hawako tayari kuona nchi ikirudi nyuma kwa sababu ya migogoro inayotokana na maslahi binafsi.
Wananchi hao kwa pamoja wametoa wito kwa Watanzania wote kuacha kutumika kama daraja la kuvuruga amani kwa ajili ya maslahi ya watu wachache.
Social Plugin