Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAIPELEKA NIDA KIDIGITALI KURAHISISHA UTOLEWAJI WA VITAMBULISHO




Na Mwandishi Wetu,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amezindua namba maalumu, itakayotumiwa na wananchi kufuatilia kitambulisho cha taifa baada ya kuwasilisha maombi ya kitambulisho hicho, hali itakayopelekea wananchi kupata na kujua taarifa za maombi ya kitambulisho kwa kutumia namba maalumu hiyo.

Amezindua namba hiyo maalumu, leo jijini Dar es Salaam, ambapo amesema vitambulisho vingi vimezalishwa na tayari vimepelekwa sehemu husika, ikiwemo wilayani ambapo muombaji wa kitambulisho alijiandikishia na bado wahusika awajafuata kadi zao hali inayopelekea baadhi ya wananchi kukosa huduma mbalimbali huku akizitaja huduma za afya, mafao ya ustawi, usajili wa wanafunzi katika vyuo mbalimbali samabamba na maombi ya mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB).

“Hivi leo tunavyozungumza katika wilaya zetu zote nchini, viko vitambulisho vingi sana ambavyo havijachukuliwa na sababu kubwa inakua kwamba muombaji hajui kitambulisho chake kipo katika hatua gani, kupitia mfumo huu ambao ninauzindua utajibiwa na utaambiwa kama namba yako umepata ndani ya siku tano na kama ujapata ndani ya siku tano tangu ulipoomba ukitumia mfumo huu(15274) utajibiwa kwanini ujapata.”Amesema Waziri Simbachawene

Ameongeza pia serikali inafikiria kusitisha matumizi ya namba ya utambulisho (NIN) kwani watu wengi wameacha kwenda kuchukua vitambulisho vyao, ambavyo vimezalishwa kwa fedha nyingi ya kodi ya watanzania, hivyo wanapaswa kwenda kuchukua vitambulisho vyao na sio kutumia namba ya utambulisho kama kitambulisho.

Akizungumza katika uzinduzi huo,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),James Kaji amesema mamlaka imeendelea kushusha vitambulisho hadi ngazi ya kata lakini bado wananchi hawajavifuata vitambulisho na wameamua kuvipeleka wilayani na anaamini sasa kupitia mfumo huo mpya wa namba 15274 vitambulisho vitaendelea kufuatwa kwani mfumo huo umerahisisha zaidi taarifa za muombaji kupatikana mkononi kiganjani kwa kupitia simu ya mkononi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com