
Matatizo yalianza baada ya kumaliza elimu ya msingi. Baraka alichaguliwa kujiunga na shule ya kutwa ya kawaida, huku Faraji akifanikiwa kwenda Shule ya Kitaifa (National School). Tangu siku hiyo, ule uzi uliowaunganisha ulikatika. Chuki ilitanda, dharau ikaingia, na mapacha hawa wakawa kama paka na panya. Nyumba ya Mzee Abdulah ilijaa huzuni na simanzi.Baada ya jitihada za kifamilia kushindikana, Mzee Abdulah alimshirikisha rafiki yake wa karibu ambaye alimuelekeza kwa mtaalamu mashuhuri, Dr. Magongo. Ingawa Mzee Abdulah alikuwa na kusitasita awali, upendo kwa wanawe ulimfanya apige hatua hiyo ya kishujaa kutafuta suluhu kwa Dr. Magongo.
Baada ya Mzee Abdulah kufuata maelekezo yote ya Dr. Magongo, anga la nyumba yake lilianza kubadilika. Siku ya kwanza ya kukutana kwao ilikuwa ya kipekee na haitasahaulika.Baraka alikuwa ameketi nje, kwenye kile kiti cha mbao ambacho mapacha hao walipenda kukaa zamani kabla ya chuki kuingia. Faraji alitoka ndani, na badala ya kupita kwa dharau kama ilivyokuwa desturi yake, alisimama ghafla na kumtazama ndugu yake. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, macho yao hayakujawa na hasira, bali yalijawa na shauku na majonzi ya kupotezana.
Faraji alikuwa wa kwanza kuvunja ukimya. Alimsogelea Baraka na kumuwekea mkono begani, ishara ambayo ilimfanya Mzee Abdulah, aliyekuwa akichungulia dirishani, kutokwa na machozi ya furaha.”Ndugu yangu Baraka, nimekukumbuka. Shule na madaraja vilitutenganisha, lakini damu yetu ni moja.”Fariji alisema (Akisimama na kumkumbatia ndugu yake kwa nguvu) Baraka alinena na kusema “Nilidhani umenisahau kwa sababu ya mafanikio yako, lakini moyo wangu ulikuwa unakuita kila siku.”
Walikaa hapo kwa saa kadhaa, wakisimuliana mambo ya shuleni na kucheka kama walivyofanya walipokuwa watoto wadogo. Ile hali ya mmoja kuhisi maumivu ya mwingine ilirejea papo hapo; Baraka alipokuwa akisimulia changamoto za shule yake, Faraji aliahidi kumsaidia kwa vifaa na maarifa aliyopata kwenye shule ya kitaifa.Tangu siku hiyo, ile kuta ya chuki ilibomoka kabisa.
Social Plugin