
Katika hatua inayoungana na wito wa amani, mfanyabiashara wa mitandaoni, Jennifer Jovin (Niffer), ambaye hivi karibuni alipata msamaha wa Rais na kuachiwa huru, ameapa kuwa balozi wa vijana ili kulinda mienendo ya vijana dhidi ya ushawishi wa vurugu na uharibifu.
Niffer amewakumbusha vijana kwamba kuna makosa mengi wanayofanya bila kujua ambayo yanapelekea hasara kubwa kwa jamii na familia. Alitoa mfano wa vurugu za Oktoba 29 zilizosababisha upotevu wa mali na maisha.
"Nitakuwa balozi mzuri wa vijana wenzangu, kuweza kulinda mienendo yetu, tunaishije, tunafanyaje na tunaepuka kipi na tunafanya kipi kwa wakati sahihi," amefafanua Niffer.
Niffer kwa kauli yake anaungana na serikali na wadau wengine wanaotambua kwamba Tanzania imebarikiwa kuwa kisiwa cha amani. na anawahimiza vijana wenzake kutunza urithi huu kwa gharama yoyote.
Aidha katika mazungumzo yake ametahadharisha kauli au matendo yanayolenga kuleta tafarani ya kitaifa.
Anahimiza wajibu wa kutunza na kuilinda miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kodi za wananchi na inafaa vizazi vijavyo. Ni wajibu wa vijana kuitunza, sio kuichoma kwa ajili ya ajenda za watu wenye nia mbaya na Taifa.
Tanzania inawahimiza Watanzania wote kuendelea kuijenga nchi kwa umoja na utulivu, bila kuruhusu wajanja wa mitandaoni kuigeuza nchi kuwa sehemu ya machafuko kwa maslahi yao binafsi.
Social Plugin