Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KISHAPU YAVUTIWA NA MAONO YA RAIS SAMIA KUHUSU MIUNDOMBINU,WIZARA YA VIJANA NA ZAO LA PAMBA


Mkazi wa mtaa wa Mhunze ya juu Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Kaifa Hija akizungumzia kuhusu hotuba ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akizindua bunge la 13 na pia kuhusu uteuzi wa baraza la mawaziri Novemba 18,2025

Na Mwandishi wetu

Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wamepongeza hotuba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 13 na kutangaza Baraza jipya la Mawaziri, wakisema imejaa dira, matumaini na mwanga mpya katika ustawi wa Taifa.

Wakitoa maoni yao Novemba 18, 2025, wananchi hao wamesema hotuba ya Rais Samia imebeba mambo muhimu yanayogusa moja kwa moja maisha ya wananchi, hususan uboreshaji wa kilimo cha mazao ya biashara ikiwemo pamba, sekta ambayo inawaingizia kipato wananchi wengi wa Kishapu.

Wamesema mipango ya Serikali kuboresha masoko, kuongeza ushindani na kuhakikisha bei ya pamba inakuwa ya haki itawainua wakulima kiuchumi, huku wakieleza kuwa hatua hiyo inaonyesha namna Rais Samia anavyowajali wananchi wa chini.

Aidha, wamepongeza kuanzishwa kwa Wizara ya Vijana, wakisema ni hatua kubwa itakayowawezesha vijana kupata fursa zaidi za ajira, ujasiriamali na kujengewa uwezo, jambo linaloendana na dhamira ya Rais Samia ya kuwekeza kwenye nguvu kazi ya Taifa.

Kaifa Hija Mkazi wa Mhunze wilayani humo amesema hotuba ya Mheshimiwa Rais imegusa kwa kina uboreshaji wa miundombinu, akitoa mfano wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Mhunze–Kolandoto. Amesema barabara hiyo ikijengwa itafungua fursa za biashara na uchumi, huku akimpongeza Rais Samia kwa kufanya uteuzi wa mawaziri kwa kuzingatia uwezo na si mazoea.

Kwa upande wake, Masunga Kazi amesema kuboreshwa kwa masoko na bei kwenye mazao ya biashara kutaleta ushindani na kuwafanya wakulima kunufaika zaidi, hasa ikizingatiwa msisitizo wa Rais juu ya kuongeza thamani ya mazao na kutengeneza ajira.

Kwa upande wake mjasiliamali wa chakula Joyce Zacharia ameeleza kuwa hotuba ya Rais imewapa matumaini makubwa wajasiriamali wadogo kwa kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara. Ameomba utaratibu wa vitambulisho vya wajasiriamali uendelee ili kuwaondolea changamoto za tozo.

Naye Paul Zachayo amesema imani kubwa ya Rais Samia kuwapa nafasi mawaziri wapya hasa vijana inaonyesha msukumo wa kusimamia uwajibikaji Serikalini. Ameongeza kuwa wananchi wanatarajia mawaziri hao kufanya kazi kwa weledi, kufuata maelekezo ya wizara zao na kuhakikisha maono ya Rais Samia yanatekelezwa kwa manufaa ya wananchi.

"Sisi wanakishapu tunatamani kuona Wizara ya Ujenzi na Kilimo zikifanya kazi kwa karibu sana wa wananchi ili kusaidia kuinua uchumi wa mtu mmojammoja na taifa kwa ujumla,tunategemea sana zao la pamba kama kiini cha zao la biashara ila tunapaswa kupata elimu zaidi na kuboreshewa mazingira ya kilimo cha umwagiliaji kupitia mto tungu tunautegemea kama chanzo cha maji ya kilimo cha mbogamboga na mahindi" Ameongeza Paul

Wananchi hao kwa ujumla wamesema wanathamini uongozi wa Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ni kiongozi anayeweka mbele maslahi ya wananchi, na hotuba yake imeonyesha dhamira thabiti ya kuendelea kujenga Taifa lenye uchumi imara, vijana wenye fursa, miundombinu madhubuti na kilimo chenye tija.
Mkazi wa mtaa wa Mnada wa Zamani Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Paul Zakayo akizungumzia kuhusu hotuba ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akizindua bunge la 13 na pia kuhusu uteuzi wa baraza la mawaziri Novemba 18,2025
Mkazi wa Mhunze Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Joyce Zacharia akizungumzia kuhusu hotuba ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akizindua bunge la 13 na pia kuhusu uteuzi wa baraza la mawaziri Novemba 18,2025
Joseph Bosi Afisa usafirishaji Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga
Mkazi wa Kijiji cha Migunga Kata ya Mwataga Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Yunge Machiya akizungumzia kuhusu hotuba ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akizindua bunge la 13 na pia kuhusu uteuzi wa baraza la mawaziri Novemba 18,2025  
Lolela Ngasa Afisa ushafirishaji Kishapu Mkoani Shinyanga

Mkazi wa Mhunze Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Masunga Kazi akizungumzia kuhusu hotuba ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akizindua bunge la 13 na pia kuhusu uteuzi wa baraza la mawaziri Novemba 18,2025
Mkazi wa Kitongoji cha Mwakija Kijiji cha Migunga Kata ya Mwataga Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Saimon John akizungumzia kuhusu hotuba ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akizindua bunge la 13 na pia kuhusu uteuzi wa baraza la mawaziri Novemba 18,2025  
Joseph Bilu Haji Afisa usafirishaji Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga









Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com