Jumla ya Wanafunzi 90 kati ya wavulana 39 na wasichana 51 wamehitimu elimu ya Kidato cha Nne mwaka 2022 katika shule ya Sekondari Nyandekwa wilayani Kahama Mkoa ni Shinyanga.

Akizungumza wakati wa mahafali Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyandekwa Melkisedeck Choya amesema Shule  hiyo ambayo ni ya kutwa na ya mchanganyiko, iliyoanzishwa mwaka 2007 ina jumla ya wanafunzi 429.