MWANAMKE AMEZWA NA CHATU

Chatu anaweza kuwa hadi urefu wa mita 10

Mwanamke mmoja nchini Indonesia ameuawa na kumezwa mzima mzima na chatu mwenye urefu wa mita 7.

Licha ya visa kama hivyo kuwa vichache hiki ndicho kisa cha hivi karibuni cha mtu kuliwa na chatu nchini Indonesia kwa takriban mwaka mmoja.
Ni kipi kilimpata mwanamke huyo?

Wa Tiba, 54, alitoweka Alhamisi iliyopita wakati akiwa kwenye shamba lake la mboga katika kisiwa cha Muna mkoa wa Sulawesi. Shughuli kubwa ya kumtafuta ilifanywa na wakaazi wa eneo hilo.

Viatu vyake na upanga vilipatikana siku moja baadaye huku chatu aliyekuwa na tumbo lililofura akipatikana mita 30 kutoka eneo hilo.

Wenyeji walishuku kuwa nyoka huyo alimuua, kwa hivyo wakamuua na kumtoa shambani.

Tumbo la nyoka huyo lilipasuliwa na mwili wa mwanamke huyo ukapatikana ndani.

Picha za kutisha zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Indonesia zikionyesha mwili wa mwanamke huyo ukitolewa tumboni mwa chatu huyo mbele ya umati mkubwa.
Chatu wanashambuaje?

Chatu wa sulawesi wanaweza kukua hadi urefu wa miaa 10 na wana nguvu sana, Wanashambulia kwa kuvizia, wakijifungia kwa windo lao na kulivunja kwa kufinya hadi kuua.Image captionChatu anaweza kuwa hadi urefu wa mita 10

Wakati unapowadia kuwala binadamu, kizuia huwa na mabega ambayo hayawezi kuvunjika. Mary-Ruth Low mtunzaji wa mbuga za wanyamapori huko Singapore ni mtaalamu wa chatu aliambia BBC.
Wanakula wanyama wakubwa?

Kawaida chatu hula panya na wanyama wengine wadogo, lakini mara wanapofikia ukubwa fulani hukosa hamu ya kula panya tena kwa sababu ni wadogo sana.

Sasa wao huanza kuwalenga wanyama wakubwa kama nguruwe au hata ng'ombe.Image captio

Mwaka uliopita mwanamume mmoja mkoani Sumatra nchin Indonesia alifanikiwa kumshinda nguvu chatu mwenye urefu wa mita 7.8 ambaye alikuwa amemshambulia kwenye shamba lake.

Alinusurika na majeraha mabaya.
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527