MAMA AUA MTOTO WAKE KISHA KUMTUPA MTONI

Polisi Kirinyaga nchini Kenya wamemkamata Mwanamke mmoja kwa tuhuma za kumkaba shingoni mtoto wake wa miaka 5 na kisha kumtupa katika mto Rutui.

Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa Mwanamke huyo mwenye miaka 23 ambaye anaishi peke yake, baada ya kutenda tukio hilo alimtupa mwanae kwenye mto na kukaa kimya akiamini kuwa maiti ya mtoto wake itachukuliwa na maji na kupelekewa sehemu isiyojulikana.

Aidha mwili wa mtoto huyo umeonekana ukielea katika mto Rutui asubuhi ya jana June 9 na ndipo wakazi wa eneo hilo ikiwemo mtuhumiwa waliwaita Polisi na kuutoa mwili wa mtoto huyo kisha wakamkamata mtuhumiwa.

Kwa mujibu wa Polisi wa kituo cha Kirinyaga Yaya Chome amesema kuwa mwanamke huyo amefunguliwa mashitaka ya kusudio la kutaka kuua katika mahakama ya Kerugoya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527