WAZIRI MKUU APIGWA MARUFUKU KUSAFIRI NJE YA NCHI

TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA MALUNDE 1 BLOG,TUPIGIE SIMU 0757 478 553 AU 0625 918 527

Waziri Mkuu wa zamani Najib Razak na mkewe Rosmah Mansor wamezuiwa kuondoka nchini, Idara ya Uhamiaji imesema leo Jumamosi.


Taarifa ya Idara ya Uhamiaji ilitolewa muda mfupi baada ya kiongozi huyo wa zamani mwenye kashfa ya ufisadi kuandika katika Facebook kwamba yeye na familia yake wanatarajiwa kwenda ughaibuni kwa mapumziko kuanzia Jumamosi na watarejea wiki ijayo.


Katika akaunti ya Twitter Najib amesema ataheshimu amri ya kuzuiwa iliyotolewa na serikali kumtaka asiondoke nchini.


"Nimetaarifiwa kwamba Idara ya Uhamiaji imenizuia mimi na familia yangu kusafiri nje ya nchi. Naheshimu amri na nitabaki nchini na familia yangu,” ameandika Najib.


Waziri mkuu huyo aliyeondolewa kupitia sanduku la kura sasa anachunguzwa na Serikali juu ya tuhuma za ufisadi wa fedha za uwekezaji ambazo maofisa wanadaiwa kuiba zaidi ya dola za Marekani 4.5bilioni.


Inadaiwa kiasi kingine cha fedha kiliishia kwenye akaunti binafsi ya Najib katika benki.


Najib amekanusha kufanya kosa lolote na anasema fedha hizo zilitolewa na familia ya kifalme ya Saudi Arabia na kwamba alikwisharejesha.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.