Picha : WAZIRI UMMY ATOA ZAWADI YA VYAKULA KWA TAASISI 10 TANGA KWA AJILI YA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu kupitia taasisi yake ya Odo Ummy Foundation leo Jumatatu Mei 28,2018 amekabidhi vyakula mbalimbali kwa taasisi 9 za kiislamu na Magereza zilizopo Jijini Tanga ili viweze kuwasaidia wakati wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. 

Taasisi zilizopata zawadi ya vyakula ni Maawal Islam, Shamsiya (Tamta),Zaharau ,Shamsul Maarifa,Swalihina Islamic Centre, Sahare ,Kituo cha Yatima cha Answar Muslim Youth Makorora ,Kituo cha Yatima Goodwill Foundation, Tangasisi,Taasisi ya Islamia Mtupie, Chumbageni, Kituo cha Watoto wenye Ulemavu Pongwena Gereza la Maweni, Tanga.

Kila taasisi imepewa unga ngano kilo 50, sukari kilo 25, tambi mifuko 2, mchele kilo 100, maharage kilo 50, unga wa dona kilo 25, mafuta ya kula dumu la lita 25 na majani ya chai kilo 3, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 6.8. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi vyakula hivyo, Waziri Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tanga (CCM) alisema ameona atoe futari hiyo kwa kila taasisi badala ya kuwaita pamoja kufuturu nao maana wengine wanaweza kushindwa kupata fursa ya kuhudhuria lakini wakikabidhiwa wanaweza kuona namna nzuri ya kuweza kuitumia wakati wa mfungo mtukufu wa Ramadhani. 

Aidha alitoa wito kwa watu mbalimbali kujitokeza kusaidia watotoyatima yanaolelewa kwenye vituo mbalimbali na taasisi za kidini kwenye kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhani ili waweze kupata uhakika wa kupata mahitaji yao muhimu wakati wa kufuturu. 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Goodwill inayolea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu Sayyed Muhdhar alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwapatia msaada huo wa futari ambao utakuwa chachu kuweza kuondoa changamoto ambazo wanakabiliana nazo hasa kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

"Kitendo alichofanya Waziri Ummy sio jambo dogo bali ni kubwa kutokana na changamoto ambazo tumekuwa tukikabiliana nazo hasa kwenye kipindi hiki cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani kutokana na mahitaji kuongezeka..Namuomba mwenyezi Mungu ampe nguvu na kumjalia maisha marefu na pale alipotoa aweze kuongezewa ",alisema.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa na Waziri Ummy Mwalimu kwa ajili ya futari kwa taasisi 10 mkoani Tanga
Sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa na Waziri Ummy Mwalimu kwa ajili ya futari kwa taasisi 10 mkoani Tanga
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akimkabidhi vyakula/futari Mkurugenzi wa Taasisi ya kulea watoto wanaoishi kwenye Mazingira magumu ya Goodwill Sayyed Muhdhar Idarus
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi futari mmoja wa walezi wa vituo vinavyolelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu JijiniTanga 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akigawa futari kwa wawakilishi wa vituo mbalimbali na taasisi za kidini tano zilizopo Jijini Tanga wakiwemo Magereza 


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla hiyo
Sehemu ya wakuu na wawakilishi wa taasisi mbalimbali Jijini Tanga wakimsikiliza Waziri Ummy
Ustadhi wa Madrasa ya Zaharau Ustadhi Abduswamad Muhammad
akipiga dua kumshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia futari hiyo
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali mara baada ya kuwakabidhi futari

(Habari/picha kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527