Picha: MAKAMU WA RAIS BUNGE LA AFRIKA STEPHEN MASELE APOKELEWA KWA SHANGWE JIMBONI KWAKE SHINYANGA MJINI

Makamu wa rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) amepokelewa kwa shangwe Mjini Shinyanga alipofika kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

Mheshimiwa Masele aliyekuwa ameambatana na wabunge wanne akiwemo Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige,Mbunge wa Manonga Seif Gulamali,Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma Jackline Msongozi na mbunge wa Babati Vijijini mkoani Manyara Jitu Son,amefanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga leo Jumamosi Mei 26,2018.

Akizungumza katika mkutano huo,Mheshimiwa Masele aliwashukuru wananchi wa Shinyanga,wabunge kwa kuendelea kumwamini na hatimaye kufanikiwa kuwa Makamu wa rais Bunge la Afrika.

“Bila wananchi wa Shinyanga kunichagua kuwa mbunge,sidhani kama ningepata nafasi ya kuwa Makamu wa rais wa Bunge la Afrika,Niwashukuru pia wabunge kwa kunikubalia kwenda kugombea nafasi hii niliyoipata na shukrani za pekee zimwendee rais John Pombe Magufuli,Makamu wa rais,Waziri Mkuu na viongozi wote ambao mmekuwa bega kwa bega na mimi kwa kila hatua ninayopitia”,alisema Masele,

Aidha aliwaomba radhi wananchi,madiwani kwa kutoonekana jimboni kwake kwa muda mrefu na kuahidi kuwa ataendelea kushirikiano nao katika shughuli mbalimbali za maendeleo licha ya majukumu mbalimbali aliyonayo.

“Nikishukuru chama changu,niwashukuru sana pia madiwani wa manispaa ya Shinyanga,kipindi ambacho mimi sipo wanafanya kazi kwa niaba yangu kama mwenzao na mimi ndiyo daraja la manispaa yetu pamoja na bunge,

Haiwezekani mtaani kwako barabara ama mtaro umeziba uchafu unataka mbunge aje afanye kazi ya kuzibua mtaro..siyo kazi ya mbunge hiyo,diwani anafanya nini?,mwenyekiti wa mtaa anafanya nini?”

“Kila mtu mmechagua kwa jukumu lake,wakisema hakuna pesa zimekuja halmashauri,hapo ni kosa langu, lakini kama pesa zinakuja wao wanashuka chini zaidi kuhakikisha miradi tuliyokusudia inasimamiwa na inatekelezwa”,aliongeza.

“Ndugu zangu naomba mnivumilie kwa sababu nitafanya kazi zote kwa muda huo huo,jua litakapotoka na kuzama nitafanya kazi za jimbo la Shinyanga,Bunge,nchi yangu na kazi za Afrika,kwa hiyo ninaomba mnaponiona sipo mnivumilie, ninatembea na Shinyanga kichwani mwangu,mtambue ninashughulikia masuala ambayo yanapaswa kushughulikiwa na mtu mwenye nafasi ya aina flani”,

“Huwa nawaambia baadhi ya watu,..yapo maamuzi yanayoweza kufanywa na mwenyekiti wa mtaa,yapo maamuzi yanayoweza kufanywa na mheshimiwa diwani,yapo maamuzi yanafanywa na mbunge,yapo maamuzi yanafanywa na waziri,waziri mkuu,makamu wa rais na mengine yanafanywa na mwenyewe mheshimiwa rais,hivyo mimi nitashughulika na masuala ambayo mheshimiwa diwani hawezi kuyafanya,hata afanyeje hawezi kuyafanya,nitashughulika na masuala ambayo yatabadilisha maisha ya wananchi”,

“Kwa hiyo tusiangaliane,tusihukumiane kwa masuala madogo madogo,tuvumiliane,mimi nina mapungufu na hata wewe una mapungufu,tuombeane kwa mwenyezi Mungu atusaidie lakini tuvumiliane,tupendane,tupeane ushauri ili kwa pamoja tuijenge Shinyanga”

“Nataka niwaahidi mbele ya wananchi,nitakitumikia chama,nitawatumikia wananchi wa Shinyanga lakini kwa majukumu mapya niliyonayo nitawatumikia wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga na wengine wenye mapenzi mema ambao kwa dhati wamefurahi mimi kupata nafasi hii,nitashirikiana nao kuhakikisha tunapiga hatua kimaendeleo kwenye maeneo yetu”,alisema Masele.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mheshimiwa Stephen Masele akiwasalimia wakazi wa Shinyanga katika eneo la Buhangija Kona mjini Shinyanga wakati akiwasili Mjini Shinyanga leo Jumamosi Mei 26,2018 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mheshimiwa Stephen Masele akisalimiana na wakazi wa Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika akiwasili katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga kwa ajili ya mkutano wa hadhara
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika akizungumza na wakazi wa Shinyanga katika Viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga
Wananchi wakimsikiliza mbunge wao
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika akizungumza na wakazi wa Shinyanga
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika akizungumza na wananchi
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika akiwahutubia wakazi wa Shinyanga
Meza kuu wakimsikiliza Mheshimiwa Stephen Masele 
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Charles Sangura akitambulisha viongozi mbalimbali wakati wa mkutano huo
Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige ambaye ni mwenyekiti wa  wabunge wa mkoa wa Shinyanga akimpongeza Mheshimiwa Stephen Masele kuchaguliwa kuwa Makamu wa rais Bunge la Afrika
Mbunge wa Manonga Seif Gulamali,akimpongeza Mheshimiwa Stephen Masele kuchaguliwa kuwa Makamu wa rais Bunge la Afrika
Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma Jackline Msongozi akimpongeza Mheshimiwa Stephen Masele kuchaguliwa kuwa Makamu wa rais Bunge la Afrika
Meza kuu
Mbunge wa Babati Vijijini mkoani Manyara Jitu Son akimpongeza Mheshimiwa Stephen Masele kuchaguliwa kuwa Makamu wa rais Bunge la Afrika
Wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanajiri
Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige akishikana mkono na Mheshimiwa Stephen Masele
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma Jackline Msongozi akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige
Mheshimiwa Masele akisalimiana na mzee Mseti
Wananchi wa Shinyanga wakisalimiana na Mheshimiwa Masele baada ya mkutano kumalizika
Wananchi wakiendelea kusalimiana na mbunge wao
Mheshimiwa Masele akiondoka katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga
Mheshimiwa Masele akiondoka katika viwanja vya Zimamoto Mjini Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527