MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU MBEYA SHABIKI WA LIVERPOOL AJINYONGA TIMU YAKE KUFUNGWA

Mwanafunzi wa mwaka wa pili Chuo kikuu cha ‘St. Augustine’ kampasi ya Mbeya Moses Mashaka amejinyonga mara baada ya timu yake ya Liverpol kushindwa kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani ulaya.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Jijini Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi Mussa Taibu wakati akizungumza na eatv.tv ambapo amesema Moses (24) amejinyonga mara baadaya ‘kubet’ na timu yake kushindwa kutwaa ubingwa.

“Mwanafunzi wa chuo kikuu cha sauti mwaka wa pili anachukua shahada ya ualimu amefariki baada ya ‘kubet’ pesa ambazo hazijulikani ni kiasi gani na baadaya Liverpol kushindwa ndipo akachukua uamuzi huo”,amesema kamanda Taibu.

Aidha Kamanda Taibu amewataka wanafunzi kuacha kutumia fedha za wazazi kwa mambo yasiyohusiana na masuala mazima ya elimu, kwani matokeo yake ni hasara kwa wazazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527