WEMA SEPETU ALIZA WATU MTANDAONI

Staa wa bongo movies Wema Sepetu amewaacha watu katika mshangao na kuchanganyikiwa baaada ya kuweka post ya kusikitisha inayohusu mwanamke ambaye alipata tatizo la kuharibika kwa mimba.


Watu wamekuwa wakijiuliza je post hiyo inamkumbusha mimba iliyoharika kipindi cha nyuma au ni mimba nyingine imeharibika tena.

Watu wengi wameonekana kuguswa na jambo hilo na kusema kuwa Wema anapitia kipindi kigumu sana kwa sasa kutokana na hamu yake kubwa ya kutaka kuwa na mtoto lakini inashindikana.

Wema aliweka picha hiyo katika ukurasa wake wa instagram na kuandika “Story of my life”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527