WAZIRI WA AFYA AZINDUA UGAWAJI WA VYANDARUA VYENYE DAWA YA MUDA MREFU KIGOMA

WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  ameagiza Waganga Wakuu Wa Mikoa,Wa Wilaya na Waganga Wafawidhi kuweka  Matangazo katika Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali kwamba huduma za 
upimaji na Matibu ya Malaria ni bure na Wananchi hawatakiwi kulipia  kwa kuwa kuna wafadhili wanao gharamia gharama hizo. 

Maagizo hayo aliyatoa leo Mkoani Kigoma katika Zahanati ya Mwandiga Wakati  akizindua ugawaji wa Vyandarua endelevu vyenye dawa ya Muda mrefu ,kwa  Wakina Mama wajawazito na Watoto wenye umri wa Mwaka Moja wa ushirikiano
wa Serikili ya Tanzania kupitia wizara ya afya kitengo cha kudhiti 
malaria na Shirika la misaada la marekani (USAID) ambapo alipokea  Malalamiko kutoka kwa Wananchi wakidai kutozwa fedha kwaajili ya  Matibabu na Wakati serikali imeagiza Zoezi hilo ni bure. 


Waziri Mwalimu alisema Ugawaji endelevu wa Vyandarua ni mradi unaoendeshwa kwa pamoja na shirika la JohnsHopkins Center for Communication na  Vectorworks kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani (USAID)  kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti malaria Na kuratibiwa na 
Serikali kupitia Mradi wa Kupambana na Malaria NMCP kwa hiyo vyandarua  hivyo ni bure na Wananchi wanatakaiwa wasilipie. 

Aidha alisema ofisi ya takwimu (NBS) katika kaya mwaka 2017 zilionyesha  kupungua kwa kiwango cha Maambukizi ya Malaria hadi chini ya asilimia  10% kutokana na Mikakati iliyowekwa na Wizara kuhakikisha wanatokomeza  ugonjwa wa Malaria. 

Alisema mikakati ya Serikali ni kuongeza kasi ya upimaji wa Malaria kwa kutumia kipimo cha (mRDT)  Hadubini na Kutumia dawa za mseto pindi wanapothibitika kuwa na Vimelea 
vya malaria , kuwapatia Wajawazito Vyandarua vyenye viuatilifu ili  kujikinga kuumwa na Mbu pia kuwapatia dawa za Sp kwa kipindi maalumu  wakati wa ujauzito ilikuwakinga na madhara yatokanayo na Malaria. 


"Niendelee Kusisitiza dawa za malaria na Matibabu ni bure Wananchi hawatakii  kulipia, wafadhiri wetu wanajitoa sana kuhakikisha Suala la Malaria  liishe , Waganga wafawidhi wanatuangusha sana niombe muweke matangazo na
namba za simu kwenye vituo vya Afya iliwananchi watakao lipishwa watoe  Malalamiko yao ilikuweza kuondokana na changamoto ya Ugonjwa wa  Malaria", alisema Mwalimu. 

Kwa upande wake Mganga  Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Vijijini , Elisha Robarti alisema zahanati hiyo
inakabiliwa na upungufu wa Watumishi wahitaji ni watumishi 15 na  waliopo ni watumishi saba hali inayopelekea Watumishi kulemewa. 

Wakitoa Malalamiko yao Wananchi waliofika kupata huduma Katika Zahanati hiyo  mbele ya Mh Waziri, Lydia Leonard alisema Wamekuwa wakitozwa shilingi  2500/= kwaajili ya Kipimo cha Malaria na kulipa dawa wanapofika kwaajili
ya Matibabu . 

Alisema pamoja na kuwa na Kadi ya  bima ya Afya lakini bado wanaendelea kutozwa fedha na kumuomba Waziri 
kusimamia suala hilo iliwaweze kupata Matibabu bure kama serikali inavyo elekeza. 

Hata hivyo Wananchi hao Shukuru Issa 
aliomba Serikali kuwajengea Kituo cha Afya Kata ya Mwandiga pamoja na  kuboreshewa huduma Za Maji kwani maji wanayo yatumia sio salama na  Wanalazimika kutumia Kilomita 13 kufuata huduma na Waziri alitoa  maelekezo kwa halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Vijijini kuanza ujenzi wa  kituo hicho kwakuwa kata hiyo inawatu wengi na inahitajika kupata kituo 
cha Afya.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ''Vyandarua bure kwa Wajawazito na Watoto,atakaeuza kukiona''.Waziri Ummy  akizungumza leo kwenye ugawaji wa Vyandarua katika Zahanati ya Mwandiga
mkoani Kigoma.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Mwantum Mohammed baada  ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda 
mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja,  mpango ambao unaendeshwa na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa  Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa  Marekani wa kupambana na Malaria. Kulia ni mwakilishi wa USAID Tanzania 
Andy Karas.
Mwakilishi wa USAID Tanzania Andy Karas akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda  mrefu Asha Juma baada ya uzinduzi wa ugawaji endelevu wa vyandarua 
vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri  wa mwaka mmoja, mpango ambao unaendeshwa na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria. 
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akiwasikiliza akinamama wanaudhuria kliniki kwenye Zahanati ya Mwandinga Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kuzindua ugawaji endelevu wa  vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto 
wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendesha na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Raisi wa Marekani wa kupambana na Malaria.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akiwasikiliza akinamama wanaudhuria kliniki kwenye Zahanati ya Mwandinga Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu 
wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na  watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendeshwa na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Raisi wa Marekani wa kupambana na Malaria.
WAZIRI Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Mwantum Mohammed baada  ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda 
mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja  mpango ambao unaendesha na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na Malaria. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527