WAZIRI : TFF HAIPO JUU YA SHERIA

Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza imesema Shirikisho la soka nchini TFF limesajiliwa chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano hivyo shughuli zake zote zipo chini ya serikali.



Mh. Shonza ameyasema hayo jana wakati akjibu swali la mbunge wa Singida Mjini Mussa Ramashani Sima ambaye alihoji kuhusu mamlaka ya Waziri katika kusimamia kazi za TFF ikiwemo mapato na matumizi ya shirikisho hilo kutokana na katiba ya TFF kutoruhusu kuingiliwa na serikali.


''TFF pamoja na viongozi wake wote, wanapaswa wanalazimika na hivyo wanatambua mamlaka ya Waziri, kwasababu katiba ya TFF inatambua kuwa TFF ni chombo cha mpira ambacho kimesajiliwa chini ya sheria ya Baraza la Michezo ya 1967 na marekebisho yake ya mwaka 1971'', alisema Shonza.


Aidha Mbunge Mussa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Singida amemuomba Waziri kuhakikisha wanaibana TFF ili ipeleka mpango kazi kwenye vyama vya mikoa ili kujua matumizi ya pesa za ruzuku zinazotolewa kwa shirikisho hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527