SINGIDA UNITED YAIKALISHA YANGA KWA KICHAPO CHA MAANA

Timu ya Yanga SC imeshindwa kusonga mbele katika michuano ya kombe la Shirikisho baada ya kuchapwa na wapinzani wao Singida United kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kutoka sare ya mabao 1-1 kwenye dakika 90 za mchezo mzima.

Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza katika mchezo huo timu ya Yanga ilifanikiwa kupata bao lake la kwanza kupitia mchezaji wake Yusuf Mhilu kwa kutumia mpira wa kichwa akiunganisha kona ya Ibrahim Ajib Kayika kwenye dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza cha mchezo na kupelekea timu yake kuongoza kipindi chote cha kwanza mpaka kuisha licha Singida United kuonesha jitihada za kutaka kusawazisha bao hilo lakini kwa bahati mbaya juhudi zao hazikuweza kuzaaa matunda.

Dakika 45 za pili za mchezo huo, Singida United walifanikiwa kusawazilisha bao la wapinzani wao kupitia mchezaji wao Kenny Ally na mpaka kipinga cha mwisho kinapulizwa timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 1-1 na kusababisha kupigwa mikwaju ya matuta na kuifanya Singida United kutoka kifua mbele baada ya kupata mikwaju 4-2 dhidi ya wapinzani wao Yanga SC.

Kutokana na ushindi huo, timu ya Singida United imejikatia tiketi ya moja kwa moja ya kuchuana na JKT Tanzania katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho.

Timu ya Yanga kwa sasa itakuwa imebakia na taji moja mkononi inalowania katika msimu huu wa mwaka 2018/2019 baada ya kutolewa leo katika michuano ya kombe la Shirikisho na Singida United kwenye dimba la Namfua mkoani Singida.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527