RAIS ASAINI SHERIA YA PEDI BURE KWA WANAFUNZI WA KIKE


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesaini muswada wa sheria ambao sasa utakuwa kamili, inayoitaka serikali kugawa pedi bure kwa wanafunzi wa kike nchini humo.

Rais Kenyatta amesaini sheria hiyo jana Aprili 10, ambayo pia inaitaka serikali kuweka mazingira salama kwa wanafunzi hao kuweza kuhifadhi pedi zao.

“Sheria ya Marekebisho ya Elimu ya Msingi, kuweka wajibu wa kutoa taulo za usafi (pedi) za kutosha na za ubora kwa kila mtoto msichana aliyesajiliwa na kujiandikisha katika taasisi ya elimu ya msingi ya umma na kufikia ujira, kwa serikali”, imesema taarifa iliyotolewa na serikali ya Kenya kwa vyombo vya habari.

Ripoti ya UNESCO ya mwaka 2016 imeeleza kwamba binti mmoja kati ya 10 kwenye nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara, anakosekana shuleni kwa siku ambazo yupo kwenye hedhi, kutokana na kukosa pedi za kujistiri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527