KAULI YA MAMA KANUMBA MAADHIMISHO YA MIAKA 6 KIFO CHA KANUMBA THE GREAT LEO

Wadau wa tasnia ya filamu na familia ya marehemu Steven Kanumba 'Kanumba the Great' leo wanaadhimisha miaka sita tangu kufariki kwa msaanii huyo.


Mama yake Flora Mtegoa, amesema yeye kwake msiba huo bado upo kila siku na kudai kila nafsi itaonja mauti.


Mtegoa ameyasema hayo leo Aprili 7,2018 katika makaburi ya Kinondoni ambapo walifanya ibada fupi kwa ajili kumbukumbu hiyo akiwa na baadhi ya wasanii hususani wa kikundi cha Soweto ambao ndio wameisimamia shughuli hiyo kwa mwaka huu.


Amesema pamoja na kujitokeza kwa wasanii wachache ambao waliwahi kufaya kazi na mtoto wake enzi za uhai wake anaamini ni kutokana na wao kuona wameshamaliza msiba, lakini kwake upo kila siku na kamwe hauwezi kufutika mpaka mwisho wa uhai wake.


"Ni kweli idadi ya wasanii maarufu waliokuja hapa ni wachache ukilinganisha na namna Kanumba alivyoishi nao, lakini ndio hivyo huwezi kuwalazimisha na isitoshe wao labda wanaona wamemaliza msiba lakini kwangu bado upo ila ninachowaombea yasije yakawakuta kama haya ndio watajua nini namaanisha,’’ amesema Mama Kanumba.


Wito wake kwa wasanii Mama Kanumba amewashauri kuwa na upendo kauli ambayo Kanumba alikuwa anapenda kuisema enzi za uhai wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527