JINSI WANAWAKE WALIOTELEKEZWA WALIVYOGEUKA "DILI' KWA MAKONDA

Unaweza kusema mgeni njoo mwenyeji apone. Ndivyo inavyotokea muda huu nje ya ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kuibuka kwa wafanyabiashara wanaowauzia chai na vitafunwa wanawake wenye watoto ‘waliotelekezwa’ na waume zao.


Wanawake hao tangu juzi wamekuwa wakiripoti katika ofisi hizo kupata msaada wa kisheria baada ya kutelekezwa na waume zao.

Leo Jumatano Aprili 11, 2018 MCL Digital imepiga kambi kuanzia saa 12 asubuhi na kushuhudia wafanyabiashara hao ndogondogo wakiwauzia chai na vitafunwa wanawake waliofika katika ofisi hizo.

Wanawake kwa vijana waliobeba chupa za chai na uji walionekana kuhudumia eneo hilo huku wengine wakiwa na ndoo za vitafunwa.

Wenye watoto walihangaika kuwapatia chochote wakati wakisubiri wanasheria wa walioandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa waanze kuwasikiliza.

Mmoja wa wafanyabiashara Salim Juma amesema zoezi hilo limeleta neema kwao.

"Tulikuwa tunazunguka mtaani kutafuta wateja ila ndani ya siku mbili hizi mambo mazuri mzigo unaisha hapa hapa," amesema Salim anayeuza vitumbua.

Na Elizabeth Edward,Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527