HAJI MANARA : WOTE NI MAKADA WA CCM LAKINI MIMI NI MAARUFU KULIKO HUMPREY POLEPOLE

Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameweka wazi kuwa yeye ni maarufu zaidi nchini Tanzania kuliko Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole.


Haji Manara amesema kuwa yeye ni kada mzuri wa CCM na Polepole anafanya kazi kama yake lakini hana jina kubwa kumzidi yeye kutokana na historia ya maisha yake na chama hicho.


Manara amedai kuwa CCM ndio chama kilichomsomesha nje ya nchi kuhusu masuala ya propaganda na ameshawahi kuwa Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Dar es salaam miaka ya 2007/10.


“Kwa upande wa siasa mimi ni mwanachama wa CCM haswa, nilikuwa Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam uongozi wangu ulikuwa 2007/10 

" Ilitokea tatizo ambalo ilibidi ifunguliwe kesi ya jinai kwangu, ilivyotokea nikafikiri 2010 tunaelekea kwenye uchaguzi na mimi ni msemaji wa chama changu cha CCM ndani ya Mkoa ndipo nikaamua kuandika barua ya kujiuzulu,“ameeleza Haji Manara kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV na kumtaja Polepole.


“Wote ni Makada wa CCM ila mimi ni maarufu zaidi, sisemi kwa kudhihaki mimi na Humphrey Polepole mimi maarufu, mimi ni kada wa Chama cha Mapinduzi na nimesomeshwa na CCM kwa wachina, kuhusu Propaganda na nikikuambia hiki kikombe ni Kamera lazima utakubali ,“amesema Haji Manara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527