Breaking News: MMILIKI WA MABASI YA HBS NA SABENA AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI

TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA MALUNDE 1 BLOG,TUPIGIE SIMU 0757 478 553 AU 0625 918 527


Basi la HBS
Basi la Sabena

Mfanyabiashara anayefahamika kwa jina la Sultan Ahmed au maarufu Chapa mmiliki wa kampuni ya mabasi ya HBS na Sabena amejipiga risasi mdomoni na risasi kutokea nyuma kichwani 'kisogoni'. 


Tukio hilo limetokea leo Jumatano Aprili 11,2018 saa tatu asubuhi  ambapo mfanyabiashara huyo mwenye asili ya kiarabu ambaye ni  lakini pía ni mmiliki wa kituo kikubwa cha uuzaji wa mafuta ya petroli wilayani Sikonge amejipiga risasi akiwa nyumbani kwake huko wilayani Sikonge mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora SACP Wilbroad Mutafungwa amethibitisha tukio hilo na kwamba wanafanya uchunguzi juu ya mauaji hayo.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Theme images by rion819. Powered by Blogger.