Updates : LOWASSA ARUDI TENA MAHAKAMANI,MGEJA NAYE AIBUKA...VIGOGO WA CHADEMA BADO HAWAJAFIKISHWA MAHAKAMANI


Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amerejea tena mahakamani mchana huu akiwa na Hamis Mgeja.

Awali, Lowassa na Sumaye waliondoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya muasisi wa Chadema, Victor Kimesera.

Hadi mchana huu watuhumiwa wote wakiongozwa na Mh. Freeman Mbowe ambao wapo gerezani Segerea waliokuwa waletwe Kisutu, hawajaletwaWakati waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa akirejea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, viongozi sita wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe bado hawajafikishwa mahakamani.

Viongozi hao wa Chadema walitarajiwa kufika mahakamani hapo mapema leo, lakini hawakufikishwa asubuhi kama tulivyoripoti awali.

Lowassa na waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye walifika mahakamani hapo leo asubuhi Machi 29, 2018 kabla ya kuondoka saa chache baadaye kwenda katika mazishi ya muasisi wa Chadema, Victor Kimesera.

Saa 8:00 mchana, mawakili wa pande zote wameingia chumba namba moja cha mahakama hiyo kumsubiri hakimu mkazi mkuu, Wilbard Mashauri.

Mbowe na wenzake wanapaswa kusomewa uamuzi na hakimu kama watapata dhamana au la, huenda uamuzi huo ukasomwa bila wao kuwapo kwa kuwa mpaka sasa hawajafikishwa.

Viongozi hao wa Chadema wanakabiliwa na makosa manane, likiwamo la kuhamasisha uasi, chuki na maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Viongozi wengine wanaokabiliwa na mashtaka hayo ni katibu mkuu, Dk Vincent Mashinji; mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; manaibu katibu mkuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar); na mweka hazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), Esther Matiko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527