SMARTPHONE ZAIDI KUTOLEWA KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA NYAKA NYAKA BONUS


Mshindi wa zawadi ya promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka,Agness Maganga(katikati)mkaazi wa Temeke akipokea simu aina ya TECNO R6 toka kwa Balozi wa Tigo Nyaka Nyaka, Meena Alli jana jijini Dar Es Salaam, Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia simu kwa kununua vifurushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# “. Anayeshuhudia ni Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama
Mshindi wa zawadi ya promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka, Farashuu Hasaan (katikati) mkaazi wa Zakhem akipokea simu aina ya TECNO R6 toka kwa Balozi wa Tigo Nyaka Nyaka, Meena Alli jana jijini Dar Es Salaam, Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia simu kwa kununua vifurushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# “. Anayeshuhudia ni Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama. 
Mshindi wa zawadi ya promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka, Issa Salum (katikati) mkaazi wa Mbagala akipokea simu aina ya TECNO R6 toka kwa Balozi wa Tigo Nyaka Nyaka, Meena Alli jana jijini Dar Es Salaam, Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia simu kwa kununua vifurushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# “. Anayeshuhudia ni Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama.
Mshindi wa zawadi ya promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka, Samwel Kivuge (katikati) mkaazi wa Mbagala maji matitu akipokea simu aina ya TECNO R6 toka kwa Balozi wa Tigo Nyaka Nyaka, Meena Alli jana jijini Dar es Salaam, Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia simu kwa kununua vifurushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# “. Anayeshuhudia ni Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama 

***
Dar es Salaam, Marchi 2, 2018 – ‘Wateja 84 wa Tigo wiki hii wamejishindia simu za Smartphone aina ya TECNO R6. Hii ni Droo ya nne ya Promosheni inayoendelea ya Tigo NYAKA NYAKA inayowawezesha wateja wa Tigo kujishindia simu mpya za kisasa zenye uwezo wa 4G na jumla ya simu 12 utolewa kwa kila siku.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama alisema “Hii ni sehemu ya kuwawezesha wateja wetu waweze kutumia simu za kisasa zenye uwezo wa 4G ili wafuruhie kuperuzi intaneti na kuweza kuangalia mambo mbalimbali kwenye simu zao”.

Aliongeza “Wateja wa Tigo Tanzania wanazidi kupata faida lukuki ikiwemo bonasi za hadi GB 1 bure kwa matumizi yao ya intaneti pamoja na fursa ya kushinda mojawapo ya simu janja 800 ambazo bado zinashindaniwa katika Nyaka Nyaka Bonus, promosheni murua inayowazawadia wateja wa Tigo wanaounua vifushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# ".

Kwa upande wa washindi mzee Issa Salum mkaazi wa Mbagala alisema “Sikuwa naamini mara baada ya kupigiwa simu nilijua matapeli wa mjini wenye kurubuni watu, baadae nikaamini nilipopewa maelezo yaliyojitosheleza” Naomba niseme hivi Tigo sio wababaishaji ni ukweli mtupu na nawashukuru kwa zawadi hii ya simu ya kisasa itakayoniwezesha kupiga picha na matumizi mengine mengi,alisema.

Naye, Farashuu Hassan mkaazi wa Mbagala alisema “Nilikuwa natumia simu yangu ndogo isiyokuwa na uwezo wa intaneti lakini sasa nimepata simu yenye uwezo mkubwa wa 4G ya TECNO R6, itakayoniwezesha kuingia kwenye Instagram, WhatsApp na kadhalika ili niwe wa kisasa kwenye ulimwengu wa mtandao”.

‘Washindi wetu wote 240 tuliowapata kufikia sasa wanatoka sehemu mbali mbali za nchi, kwa hiyo ninawashauri wateja wetu kote nchini washiriki ili wajishindie bonasi za data bure pampoja na mojawapo ya simu zaidi ya 800 za Smartphones ambazo bado zinashindaniwa,’ Bushagama alisema. 

Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527