WAOMBOLEZAJI WAPORWA MABANGO WAKIAGA MWILI WA MWANAFUNZI ALIYEPIGWA RISASI DAR


Baadhi ya waombolezaji ambao walijitokeza kuaga mwili wa marehemu Akwilina aliyekuwa anasoma katika Chuo Cha Usafirishaji (NIT ) jijini Dar es Salaam wamepokonywa mabango mbalimbali ambayo yalikuwa na jumbe mbalimbali kuhusiana na kifo hicho. 

Waombolezaji hao ambao wengine walikuwa wameshika mabango kuhoji uhalali wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba na IGP Sirro kuendelea kuwepo ofisini mpaka sasa licha ya mauaji hayo kutokea.

Walijitokeza vijana mbalimbali ambao walikuwa wamevaa suti nyeusi na kuanza kupokonya mabango hayo kwa waombolezaji hao na kuondoka nayo, tukio hilo limetokea wakati Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako akihutubia mamia ya waombolezaji katika Viwanja vya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT).

Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527